Mbabe Cheka |
Na Prince Akbar
KAMISHENI ya
Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) tayari imemtafutia bondia Francis Cheka mpambano
wa marudiano kati yake na bondia Chiotra Chimwemwe wa Malawi katika jiji la
Addis Ababa, Ehtiopia.
Mpambano huo
utafayika January 26, siku ya ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa nchi za Africa
(AU Summit) katika jiji hilo la Wafalme la Abesinia!
Cheka na
Chimwemwe watakutana jijini Arusha Desemba 26 (Boxing Day) katika mpambano wa
kutafuta nani mbabe wa uzito wa Super Middle katika bara la Afrika, Mashariki
ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG). Katika mpambano huo mafahali hawa
wawili wataumana kiume kwa raundi 12 za dakika tatu kila mmoja!
Mpambano wa
Cheka na Chimwemwe jijini Arusha umeandaliwa na kampuni ya Screen Hills (T)
Investment ya jijini Dar-Es-Salaam inayomilikiwa na promota maarufu aliyewahi
kuwa bingwa wa taifa katika ngumi za ridhaa na kulipwa Andrew George aka Chagga
Boy!
Umaarufu wa
wawili hawa umewafanya mapromota wanaoandaa tamasha la kuchangisha pesa kwa
ajili ya kulisha watu wenye njaa katika bara la Africa kuwaingiza Cheka
26(15)-6(3)-1 na Chiotra 26(15)-4(2)-1 katika mpambano hwa marudiano
utakaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 26 Januaru 2012!
Katika
tamasha hilo, pambano kuu litakuwa kati ya bondia Oliver McCall 56(37)-12(1)-0
kutoka Marekani ambaye aliwahi kuwa bingwa wa uzito wa juu duniani akipambana
na bondia Sammy Retta - 18(17)-3(2)-0 kutoka Ethiopia kugombea ubingwa wa IBF
Africa, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa juu
(Heavyweight)
Mapambano
mengine yatawakutanisha mabondia Daniel Wanyonyi 14(12)-5(2)-2 wa Kenya
atakayechuana na bondia Issac Hlatswayo 30(10)-5(3)-1 kutoka Afrika ya Kusini
katika kugombea ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi
(IBF AMEPG) katika uzito wa Welterweight
Naye Manzur
Ali 7(4)-8(3)-0 bingwa wa uzito wa juu kutoka nchi ya Misri atachuana vikali na
bondia Harry Simon 27(20)-0-0 kutoka Namibia ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki
ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa Light heavyweight.
Mpambano huu
umeidhinishwa na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) na Cheka kupewa kibali
na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC).