// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CANNAVARO AWATANGAZIA HALI YA HATARI KILI STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CANNAVARO AWATANGAZIA HALI YA HATARI KILI STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, December 07, 2012

    CANNAVARO AWATANGAZIA HALI YA HATARI KILI STARS

    Cannavaro katikati akimbkimbilia Aggrey Morris kushangilia naye baada ya kufunga bao la pili jana. Kulia ni Khamis Mcha 'Vialli'

    Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
    NAHODHA wa Zanzibar, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kwamba wameumia sana kufungwa na Kenya jana, lakini wanafuta machozi na kuelekeza nguvu zao kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Tanzania Bara kesho.
    “Kwa kweli tumeumia sana, ila ndio mpira, kama mlivyoona, tulipigana kadiri ya uwezo wetu, ila bahari haikuwa yetu,”alisema Cannavaro.
    Hata hivyo, Cannavaro alisema kwamba nia pekee ya kuwafariji Wazanzibari na kushinda mechi ya kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Bara kesho.
    “Utakuwa mchezo mgumu, lakini tutapigana kuwafunga kwa sababu haitakuwa mara ya kwanza sisi kuwafunga wao,”alisema.
    Zanzibar ilikufa kiume jana, baada ya kutolewa kwa penalti 4-2 na Kenya katika Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika ya 120.
    Hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, Zanzibar wakitangulia kupata bao dakika ya 20, mfungaji Khamis Mcha ‘Vialli’, aliyeunganisha pasi ya Jaku Juma, baada ya kazi nzuri ya Suleiman Kassim ‘Selembe’.
    Kenya ilisawazisha dakika ya 29, mfungaji Mike Barasa ambaye alifumua shuti lililowachanganya Nahodha, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kipa wake, Mwadini Ally na kutinga nyavuni.
    Zanzibar waliuanza vizuri mchezo huo na kusukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Kenya kutokea pembeni, ambao walionekana kabisa kuzidiwa na kutumia muda mwingi kucheza kwa kujihami.
    Hata hivyo, baada ya kupata bao la kusawazisha, kibao kiliwageukia Wazanzibar na kuanzia hapo Kenya ndio waliokuwa wakisukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa wapinzani wao.
    Kipindi cha pili, mchezo ulianza kwa kasi na Zanzibar walionekana kucheza kwa tahadhari wakiwadhibiti Wakenya, huku wakiendelea kumiliki zaidi mpira.
    Hali hiyo ilizaa matunda ya Heroes kupata penalti dakika ya 75 baada ya mshambuliaji Juma Jaku kuangushwa kwenye eneo la hatari, Joackins Atudo, wakati anakwenda kumuona kipa Duncan Ochieng na refa Thierry Nkurunzinza wa Burundi akaamuru pigo hilo.
    Nahodha Aggrey Morris alikwenda kupiga penalti hiyo na kuikwamihsa kimiani kuipatia bao la pili Zanzibar.
    Hata hivyo, bao hilo halikudumu sana, kwani dakika ya 80 Kenya walisawazisha kupitia kwa Mike Barasa tena, akiunganisha krosi ya Paul Were aliyeingia kuchukua nafasi ya Ramadhan Mohamed dakika ya 46.    
    Hadi dakika 90, timu hizo zilikuwa zimefungana 2-2 na mchezo ukahamia kwenye dakika 30 za nyongeza, ambako Kenya walishinda.
    Khamis Mcha ‘Vialli’ alikosa penalti ya kwanza kabisa na Issa Othamn Ally akakosa ya pili, wakati Aggrey Morris na Samir Hajji Nuhu walifunga. Kwa upande wa Kenya, waliofunga ni Mike Barasa, Joackins Atudo, Edwin Lavatsa na Abdallah Juma aliyepiga ya mwisho.
    Kwa ushindi huo, Kenya itacheza Fainali na mshindi wa mechi ya pili kati ya Uganda na Tanzania, wakati Zanzibar itawania nafasi ya tatu dhidi ya timu itakayofungwa usiku huu.
    Kenya; Duncan Ochieng, Anthony ‘Modo’ Kimani, Joackins Otieno Atudo, David Owino Odhiambo, Abdallah Juma Baya, David Ochieng, Kevin Omondi Obwaka, Humphrey Ochieng Mieno, Clifton Miheso Ayisi/Paul Were Ooko, Ramadhan Mohamed Salim/Edwin Lavatsa Jumba na Mike Baraza.
    Zanzibar; Mwadini Ally, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Nassor Masoud ‘Chollo’, Samir Hajji Nuhu, Aggrey Morris Ambroce, Sabri Ally Makame, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Khamis Mcha ‘Vialli’, Jaku Juma Jaku/Abdallah Othman Ally, Amir Hamad Omar na Adeyom Saleh Hemed/Seif Rashid Abdallah.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: CANNAVARO AWATANGAZIA HALI YA HATARI KILI STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top