Okwi |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
EMANUEL
Okwi, mshambuliaji tegemeo wa Uganda, amesema kwamba ukuta wa Tanzania Bara ni
mzuri na kuupita ni kazi, lakini akaapa kesho watafanya kila wawezalo
kuhakikisha wanaupenya na kufunga.
Akizungumza
na BIN
ZUBEIRY jana, Okwi alisema kwamba wachezaji wote wa safu ya ulinzi ya
Stars wana akili na nguvu za kupambana na mshambuliaji wa aina yeyote, hivyo
keso itakuwa kazi sana.
“Inahitaji
maarifa sana kuweza kupenya pale, Shomary (Kapombe) ni mchezaji mwenye akili
sana na anajituma, Yondan (Kevin), pia ana akili sana, uzoefu na anajituma.
Mimi nimemkuta pale Simba hadi anahamia Yanga (msimu huu).
Na tangu
nakuja Simba yeye ni mchezaji wa timu ya taifa, wana Kaseja (Juma) kipa mzuri
na mzoefu, tena sana, kwa hivyo ukuta wao ni mzuri sana, ila na sisi tuna safu
kali sana ya ushambuliaji, Diego (Hamisi Kiiza), Brian (Umony), Ssentongo (Robert),
Kizito (Geoffrey) na mimi, wote nadhani unajua cheche zetu.
Kwa hivyo
hiyo mechi itakuwa sana, lakini sisi kwa sababu tunacheza nyumbani, inatupa
nafasi nzuri zaidi ya kusonga mbele, yote kwa yote, mchezo utakuwa mgumu, ila
kushinda sisi lazima,”alisema Okwi.
Wakati ukuta
wa Cranes haujaruhusu hata bao moja, ukuta wa Stars umeruhusu bao moja tu
katika mechi nne, dhidi ya Burundi, tena la penalti lilofungwa na Nahodha wao,
Suleiman Ndikumana, Kilimanjaro Stars ikilala 1-0.