Wachezaji wa Azam Academy wakiwa na Abedi Pele alipotembelea Azam Complex. Leo wameua 2-0. |
Na Prince Akbar
AZAM FC imeanza
vema michuano ya Kombe la Uhai, inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya
miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuilaza Mgambo
Shooting mabao 2-0 jioni ya leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Shukrani kwao,
Jamil Mchaulu ‘Balotelli’ na Reyna Mgugingila, wafungaji wa mabao hayo leo katika
mchezo huo wa Kundi B.
Katika mechi
za asubuhi, Coastal Union ya Tanga nayo ilianza vizuri baada ya kuifunga
Tanzania Prisons mabao 2-1, mchezo wa Kundi A uliopigwa Uwanja wa Karume, Dar
es Salaam.
Coastal
Union ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa tayari imepachika mabao hayo
yaliyofungwa dakika ya 24 na 33 kupitia kwa Ramadhan Same na Yusuf Chuma.
Tanzania
Prisons ambayo itacheza mechi yake pili kesho jioni (Desemba 12 mwaka huu)
Uwanja wa Azam ulioko Chamazi dhidi ya JKT Ruvu ilipata bao lake dakika moja
kabla ya filimbi ya mwisho. Mechi nyingine ya asubuhi, African Lyon iliichapa
mabao 4-0 Polisi Moro.
Mechi
nyingine za kesho ni Toto Africans dhidi ya Coastal Union itakayochezwa saa 2
asubuhi Uwanja wa Azam. Katika kundi B, Simba na African Lyon zitaoneshana kazi
asubuhi Uwanja wa Karume wakati Azam na Polisi Morogoro zitacheza saa 10 jioni
kwenye uwanja huo huo.
Kundi C
kesho ni Kagera Sugar vs Oljoro JKT saa 2 asubuhi Uwanja wa Karume, na Yanga na
Ruvu Shooting zitaumana saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Azam.