Jemedari Said, Meneja Msaidizi wa Azam akiiongopza timu mazoezini jana |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kinshasa
AZAM FC
inashuka dimbani leo kumenyana na Shark FC kwenye Uwanja wa Martyrs mjini hapa
katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi B, kuwania Kombe la Hisani,
linaloandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC).
Azam
inahitaji ushindi katika mchezo wa leo ili kwenda Nusu Fainali, kwani katika
mchezo wake wa kwanza ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Dragons pia ya
hapa Kinshasa.
Kwa kuwa
Kundi B lina timu tatu, maana yake Azam ikishinda itakuwa moja kwa moja
imefuzu, lakini hata sare itakuwa mbaya kwao, kwani Dragons na Sharks ambazo
zitakutana katika mechi ya mwisho ya kundi hilo Desemba 23, zinaweza kupanga
matokeo.
Azam
ilicheza mechi ya kwanza bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall
na Msaidizi wake, Kali Ongala ambao walibaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari
Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche raia wa Ivory
Coast, kutokana na kukosa viza za kuingia DRC, lakini wote hao wanatarajiwa
kuwasili leo mjini hapa.
Ikifuzu
kwenye kundi lake, Azam itaingia Nusu Fainali moja kwa moja, ambazo zitachezwa
Desemba 25 wakati Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa
tatu.
Kundi B,
lina timu za DC Motema Pembe, Diables Noirs, FC MK na Real De Kinshasa.
Kikosi cha
Azam leo kinatarajiwa kuwa; Mwadini Ally, Himidi Mao, Waziri Salum, Luckson
Kakolaki, David Mwantika, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Abdi Kassim, Gaudence
Mwaikimba, Humphrey Mieno na Uhuru Suleiman.