WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, Azam FC wamealikwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Desemba 13 hadi 23 mwaka huu kushiriki mashindano ya Ngao ya Jamii, yatakayofanyika mjini Kinshasa.
Kwa mujibu wa tovuti ya Azam, mashindano hayo ambayo yatashirikisha timu kubwa za kutoka Kongo kama DC Motema Pembe na A.S. Vita Club timu kutoka nje ya kongo kama Azam FC, Tusker FC ya Kenya, Gombe United ya Nigeria na Diable Noirs ya Kongo Brazavile.
Azam itayatumia mashindano kama sehemu ya maandalizi yake ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho Afrika
Azam FC, inayonolewa na Muingereza, Stewart Hall imepanga kufanya maandalizi ya uhakika kwa kucheza mechi nyingi za kujipima nguvu nje ya Tanzania ili kujiweka imara.