Atudo |
Na Mahmoud Zubeiry
BEKI wa
kimataifa wa Kenya, Joackins Atudo amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea
Azam FC ya Dar es Salaam.
Katibu wa
Azam FC, Nassor Idrissa amesema mida hii kwamba, beki huyo kutoka Tusker ya
Kenya, amekwishamalizana na uongozi wa klabu hiyo baada ya kutua leo Dar esw
Salaam.
Tayari Azam
imekwishafikia makubaliano na mshambuliaji wa Uganda, Brian Umony kusaini
mkataba wa miaka miwili, akitokea KCC ya kwao, Uganda.
Awali, Umony
alifanya mazungumzo na Simba SC ya Dar es Salaam pia na kufikia nao
makubaliano, lakini Wekundu hao wa Msimbazi kwa kitendo cha kuchelewa
kumalizamna naye, sasa ‘wanaishia kunawa’.
Umony
alikuwa pia akiwaniwa na El Merreikh ya Sudan, ambayo nayo ilituma mwakilishi
wake kwenda kuzungumze naye Uganda wiki iliyopita.
Brian
amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na KCC baada ya kumaliza mkataba wake, Becamex
Binh Duong F.C. ya Vietnam.
Mwaka 2009,
baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili
Emmanuel Okwi aliyekuwa SC Villa wakati huo.
Umony
aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya
Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa
mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C. Brian anang’ara katika Kombe
la Challenge, hadi sasa ana mabao matatu. Azam pia ina mpango wa kusajili
Wakenya wengine wawili, Jockins Atudo na Humphrey Mieno.