Taddy Etikiama |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
KLABU ya
A.P.R. ya Rwanda inataka kumsajili mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Taddy Etikiama wa A.S. Vita.
Etikiama
anayeichezea Rwanda katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA
Tusker Challenge, akitumia jina la Dadi Birori, tayari amekwishaonyesha nia ya
kujiunga na Yanga.
Habari
kutoka ndani ya kambi ya Rwanda, zimesema kwamba A.P.R. inayomilikiwa na jeshi
la nchi hiyo imevutiwa na uwezo wa mchezaji huyo na kwa kuwa amekwishamaliza
mkataba wamke Vita, inataka kumsajili.
“Huyu Dadi
APR wanataka kumsajili, akirudi tu Kigali watazungumza naye, na kwa vile
amekwishamaliza mkataba wake AS Vita, watamsajili, ni mzuri sana,”kilisema chanzo kutoka kambi ya
Rwanda, hoteli ya Sports View mjini hapa.
Mwishoni mwa
wiki, Etikiama aliwaambia Yanga SC ya Dar es Salaam, wasikosee kusajili
mshambuliaji mwingine yeyote zaidi yake, kwani yeye ndiye mkali anayewafaa
zaidi.
Akizungumza
na BIN
ZUBEIRY mijini hapa, Taddy ambaye hadi ameifungia Rwanda mabao mawili katika
Kombe la CECAFA Tusker Challenge alisema kwamba huu ni wakati mzuri Yanga
kumsajili, kwani amemaliza mkataba na klabu yake A.S. Vita ya DRC.
Alisema
anaijua Yanga vizuri na mfumo wake wa uchezaji pia na anaamini akijiunga nayo
atawafungia sana mabao. “Najua wana wapinzani wao wakubwa, Simba, mimi
nikisajiliwa Yanga nitakuwa nawafunga sana hao Simba,”alisema Etikiama na
kuongeza.
“Mimi ni
mkali kweli, nimekuwa mfungaji bora wa Kongo (DRC), nimefunga mabao 15 ligi
yenye timu nzuri kama TP Mazembe, St Eloi Lupopo na DC Motema Pembe,
nimewashinda akina Mbwana Samatta, Yanga wakinipata watapata mchezaji mzuri wa
ushindi,”alisema.
Taddy
alikuwa na A.S. Vita kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Kagame, ambayo Yanga iliibuka bingwa.
Katika
mashindano hayo yaliyofanyika mjini Dar es Salaam Taddy alikaribia kuwa
mfungaji bora baada ya kushika nafasi ya pili kwa mabao yake sita, nyuma ya
Said Bahanuzi wa Yanga aliyefunga saba na kutwaa kaitu cha dhahabu cha michuano
hiyo.
Taddy
alifunga idadi sawa ya mabao na mshambuliaji mwingine wa Yanga, Hamisi Kiiza
‘Diego‘, ambaye katika Challenge hii naye anachezea nchi yake, Uganda.