// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AKUFFO ANAWEZA KURUDI SIMBA SC 2013 IWAPO... - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AKUFFO ANAWEZA KURUDI SIMBA SC 2013 IWAPO... - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, December 17, 2012

    AKUFFO ANAWEZA KURUDI SIMBA SC 2013 IWAPO...

    Akuffo akishangilia moja ya mabao yake aliyoifungia Simba Sc

    Na Princess Asia
    MSHAMBULIAJI Daniel Akuffo kutoka Ghana, anaweza kuwa na nyota ya jaha na kujikuta anabakia kwenye kikosi cha Simba SC hadi mwakani.
    Hiyo inafuatia mipango ya klabu hiyo kusajili mshambuliaji mwingine wa kigeni baada ya kuondoka kwa Felix Mumba Sunzu Jr. hadi sasa kuwa bado haijafanikiwa.
    Akuffo alipewa tiketi ya kwenda tu kwao, lakini anaweza kutumia tiketi ya kurejea Dar es Salaam kuendelea na kazi, iwapo Simba haitapata kabisa mshambuliaji mwingine. Lakini inawezekana pia Simba ikaamua kubaki na wachezaji wanne tu wa kigeni, kutokana na Akuffo kutokubalika kabisa mbele ya baadhi ya viongozi wa Simba SC.
    Simba ilitaka kusajili mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Brian Umony lakini bahati mbaya kwao, wakazidiwa kete na Azam FC.
    Kwa sasa ni wachezaji wanne tu wa kigeni wenye uhakika wa kuichezea Simba SC katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, ambao ni Waganda, kipa Abbel Dhaira, kiungo Mussa Mudde na mshambuliaji Emanuel Okwi, pamoja na beki kutoka Mali, Komabil Keita.
    Kutoka kikosi cha Simba kilichocheza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, wachezaji Felix Sunzu kutoka Zambia, Daniel Akuffo kutoka Ghana na beki Paschal Ochieng kutoka Kenya, wametupiwa virago.
    Simba inatarajiwa kuanza rasmi mazoezi baada ya sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya, wakati kocha wake mpya, Patrick Liewig kutoka Ufaransa atapowasili.
    Liewig anayekuja kurithi mikoba ya Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick aliyetupiwa virago, ni kocha wa zamani wa Akademi ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Club Africain ya Tunisia, Patrick Liewig ndiye atakayerithi mikoba ya Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick katika klabu ya Simba.
    Liewig ana Stashahada ya Juu ya ukocha na Shahada ya tatu ya ualimu wa soka ya vijana aliyotunukiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa Ufaransa, Gerard Houiller na amehudhuria pia kozi za ufundishaji mazoezi ya viungo Juni mwaka 1999 katika Chuo Kikuu cha Dijon.
    Kwa upande wa uzoefu, Liewig alifanya kazi PSG kuanzia mwaka 1989 hadi 1999 kama Kocha Mkuu wa akademi na kuna wakati alikuwa akishirikishwa pia katika programu za timu A, ingawa majukumu yake zaidi yalikuwa ni kwa Under 20, Under 18 aliowawezesha kutwaa Kombe la French Junior Gambardella na Under 16.
    Kuanzia mwaka 1989 hadi 1990:  alikuwa Meneja Mkuu wa Tomislav IVIC, 1990 hadi 1991 alikuwa Msaidizi wa Henri Michel, 1991 hadi 1994 alikuwa Msaidizi wa Artur Jorge, 1994 hadi 1996 alikuwa Msaidizi wa Luis Fernandez, 1996 hadi 1998: alikuwa Msaidizi wa Ricardo Gomez, 1998 hadi 1999 alikuwa Msaidizi wa Alain Giresse.
    Liewig pia alifundisha Al Wahda FC ya Abu Dhabi kuanzia 1999 hadi 2001, ambayo aliipa ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo na Kombe la Ligi.
    Januari mwaka 2003 alikuwa Msimamizi wa Chama cha Soka UAE katika fainali za Afrika za U20 nchini Burkina Faso.
    Kuanzia mwaka 2004 hadi 2009 alikuwa Kocha wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast aliyoipa mataji matatu ya Ligi Kuu ya nchini humo mfululizo, 2004, 2005 na 2006, Super Cup ya nchini humo 2005, 2007, 2008 na 2009 na akaiwezesha kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa mara tatu, mara moja akiifikisha Nusu Fainali.
    Amekuwa Kocha bora wa Ivory Coast miaka mitatu mfululizo, 2004, 2005 na 2006 na tangu Septemba mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alikuwa kocha wa Club Africain ya Tunisia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AKUFFO ANAWEZA KURUDI SIMBA SC 2013 IWAPO... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top