Yaw Berko |
Na Mahmoud Zubeiry
KIPA Mghana,
Yaw Berko hataachwa katika klabu ya Yanga kama ambavyo magazeti mengi nchini
yamekuwa yakiandika.
Habari ambazo
BIN
ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba Berko ambaye
mkataba wake unamalizika Mei mwakani, ataendelea kuitumikia klabu hiyo hadi
mwisho wa mkataba huo.
Kipa huyo
anayelipwa mshahara wa Sh. Milioni 1.5 kwa mwezi, amerudishwa benchi siku za
karibuni baada ya kufululiza kufungwa mabao rahisi, jambo ambalo lilimkera
kocha Mholanzi, Ernie Brandts.
Kwa sababu
hiyo, vyombo vya habari vikaanza kubashiri kwamba ataachwa mwezi ujao kwa
sababu pia, tayari klabu hiyo imesajili mchezaji mwingine wa kigeni, Kabange
Twite kutoka APR ya Rwanda.
Kanuni za
Usajili za Ligi Kuu zinataka wachezaji watano tu wa kigeni kwa kila klabu, na
Yanga tayari inao Yaw Berko, Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima kutoka Rwanda,
Hamisi Kiiza kutoka Uganda na Didier Kavumbangu kutoka Burundi.
Lakini habari
zaidi zinasema Kabange atachukua nafasi moja kati ya mbili zinazotarajiwa
kuachwa na wachezaji wawili wa klabu hiyo, ambao watauzwa hivi karibuni, Niyonzima
na Kavumbangu.