Wafungaji wa mabao ya Yanga leo, Kavumbangu kushoto na Kiiza anayemfuatia wakiwa wametazama wakishangilia. Hii ilikuwa katika mechi dhidi ya Azam. (Picha kutoka Maktaba ya BIN ZUBEIRY) |
YANGA imeendelea kuwapa raha mashabiki wake, baada ya
kufanikiwa kumaliza vema mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara ikijishindilia kileleni zaidi, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
wenyeji Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Yanga imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 29,
ikifuatiwa na Azam FC katika nafasi ya pili yenye pointi 24 na Simba SC nafasi
ya tatu kwa pointi zao 23.
Hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0. Lililotiwa
kimiani na mshambuliaji wake wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu dakika
ya 28, kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na kiungo Simon Msuva.
Kipindi cha pili, Yanga walirejea na moto wao tena na
iliwachukua dakika 17 tu kuandika bao la pili, mfungaji Mganda Hamisi Kiiza
‘Diego’ aliyeuwahi mpira ambao aliuokosa beki wa Coastal, Mbwana
Hamisi na kuutumbukiza nyavuni kiulaini.
Yanga SC;
Ally
Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin
Yondan, Nurdin Bakari, Frank Domayo, Simon Msuva, Hamisi Kiiza, Haruna
Niyonzima na Didier Kavumbangu/Said Bahanuzi.
Coastal
Union; Juma Mpongo, Ismail Amour Khamis, Juma Jabu, Jamal
Macherenga/Othman Omar Tamim, Mbwana Hamisi, Jerry Santo, Soud Mohamed, Razack
Khalfan, Daniel Lyanga, Atupele Green/Lameck Dayton na Suleiman Kassim ‘Selembe’.