Kenya |
NYOTA WA HARAMBEE:
Sudan |
MWEWE WA JANGWANI;
TIMU
ya taifa ya Sudan inajulikana kwa jina la utani kama Sokoor Al-Jediane Kiarabu,
Kiingereza Desert Hawks, yaani Mwewe wa Jangwani. Hii ilikuwa moja ya nchi tatu
tu nyingine zikiwa ni Misri na Ethiopia zilizoasisi Kombe la Mataifa Huru ya
Afrika mwaka 1957 na ilifanikiwa kushinda taji hilo mwaka 1970, wakiwa wenyeji,
baada ya kuwafunga Ghana 1-0 kwenye fainali, wakitoka kuifunga Misri 2-1 katika
Nusu Fainali. Sudan ni miongoni mwa timu kongwe barani Afrika na ilikuwa ina
historia ya utajiri miaka ya 1950 na 1970. Sudan pia ilishika nafasi ya pili
kwenye michuano hiyo katika fainali za mwaka 1959 zilizofanyika mjini Cairo,
Misri zikishirikisha nchi tatu, yani mbali na wenyeji, pia walikuwapo Ethiopia.
Ilishika tena nafasi ya pili katika fainali za mwaka 1963 baada ya kufungwa na Ghana
3-0 kwenye fainali, wakati 1957 ilikuwa ya tatu. Sudan pia wametwaa mara tatu
Kombe la Challenge katika miaka ya 1980, 2006 na 2007 na wamekuwa wa pili mara
mbili 1990 na 1996 na washindi wa tatu mara mbili pia, 1996 na 2004.
Uganda |
KORONGO WA KAMPALA;
Uganda
ambayo timu yake ya taifa inaitwa The Cranes, yaani Korongo hawajawahi kufuzu
kwenye fainali za Kombe la Dunia, na kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika matokeo yao mazuri kabisa ni kushika nafasi ya pili mwaka 1978, baada ya
kufungwa na wenyeji Ghana 2-0 mjini Accra. Lakini Korongo wa Uganda wanajivunia
kuwa timu iliyotwaa mara nyingi zaidi taji (mara 12) Kombe la Challenge, katika
miaka ya 1973, 1976, 1977, 1989, 1990, 1992, 1996, 2000, 2003, 2008, 2009 na
2011 na pia imeshika nafasi ya pili mara nne.
Rwanda |
NYIGU WA KIGALI;
Burundi |
MBAYUWAYU WA BUJUMBURA;
Lakini
ni nchi ambayo imebarikiwa wachezaji wenye vipaji, ingawa wengi baadaye huikana
nchi hiyo na kuchukua uraia wa nchi jirani, kwa mfano Nonda Shabani aliyehamia
DRC na Hamadi Ndikumana aliyejivika Unyarwanda.
Somalia |
MABAHARIA WA MOGADISHU;
Zanzibar |
MASHUJAA WA VISIWANI;
Zanzibar
pia imewahi kuingia Nusu Fainali mara sita na mbili ikishika nafasi ya tatu,
wakati michuano ya mwaka huu, inaeonekana kuwa na kikosi imara zaidi.
Ethiopia |
SWALA DUME;
Ethiopia
ambayo timu yake ya taifa inajulikana kama The Walya Antelopes, mchanganyiko wa
maneno mawili, la Kiingereza na Kihabeshi, lenye maana ya ‘Swala dume’ ni
miongoni mwa nchi tatu pamoja na Misri na Sudan zilizoasisi michuano ya Mataifa
Huru ya Afrika mwaka 1957 na wakafanikiwa kutwaa taji hilo mwaka 1962
walipokuwa wenyeji, ingawa baada ya muongo huo, ilipoteza makali yake.
Baada
ya kuzisakosa kidogo fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2004, kwa kuzidiwa
pointi tatu tu, baada ya kufungwa na Guinea, Ethiopia mwakani itashiriki tena
fainali hizo nchini Afrika Kusini, baada ya miaka 31. Inajivunia pia kutwaa
mataji ya Challenge katika miaka ya 1987, 2001, 2004 na 2005.
Tanzania Bara |
NYOTA WA KILIMANJARO;
Haijawahi
kushiriki fainali hata moja za Kombe la Dunia, lakini inajivunia kucheza
fainali moja za mwaka 1980 za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Nigeria,
sambamba na kutwaa mara tatu Kombe la Challenge katika miaka ya 1974, 1994 na 2010
na kushika nafasi ya pili mara tano.
Malawi |
MWALE WA NYASA;
Mafanikio
yao makubwa
katika soka ya kimataifa ni kushika nafasi ya tatu katika Michezo ya Afrika
mwaka 1987. timu hiyo ambayo kwa sasa iko chini ya kocha mzalendo Kinnah Phiri,
imewahi kushika nafasi ya pili mara mbili katika michuano ya Kombe la Mataifa
ya Kusini mwa Afrika (COSAFA), wakati kabla ya kuhami huko, ikiwa bado
mwanachama wa CECAFA, ilitwaa Kombe la Challenge mara tatu katika miaka ya
1978, 1979 na 1988 na pia kushina nafasi ya pili mara tatu. Imekuja tena kushiriki
Challenge mwaka huu kama mgeni mualikwa.
Sudan Kusini |
NYOTA ANGAVU WA SUDAN KUSINI;
Sudan
Kusini, au Bright Star, yaani Nyota Angavu kwa jina la utani, huyu ni
mwanachama mpya kabisa wa CECAFA, nchi iliyojigawa kutoka Sudan ambayo sasa
inatambulika katika familia ya soka kama taifa kamili. Kwao hizi zitakuwa
fainali za kwanza kabisa za Challenge. Sudan Kusini rasmi ilicheza mechi yake
ya kwanza ya kimataifa Julai 10, mwaka huu na kutoka sare ya 2-2 na Uganda
nyumbani. Hii ni kuashiria kwamba, pamoja na upya wao si timu ya kubeza kwa
kitendo cha kutoka nguvu sawa na mabingwa watetezi wa michuano hii.
Eritrea |
WAVUVI WA BAHARI NYEKUNDU ERITREA;
Imekosekana
katika fainali mbili zilizopita za Challenge kutokana na tabia ya wachezaji
wake kuzamia nchi za watu wanapokwenda kucheza mechi. Wachezaji wanne wa klabu
ya Red Sea FC walizamia Nairobi baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa na wengine 12
wa timu ya taifa wakazamia Tanzania mwaka 2007 baada ya Challenge. Wachezaji
wengine sita walizamia Angola Machi mwaka 2007 baada ya mechi ya kufuzu ya
Kombe la Mataifa ya Afrika. Wachezaji wengine watatu zaidi walizamia Sudan,
hivyo Eritrea ikajitoa kwenye soka ya kimataifa kwa ujumla ili kutafuta dawa ya
kukabiliana na tatizo hilo na sasa serikali ya nchi hiyo inamtaka kila mchezjai
kuweka nakfa 100,000 (fedha za kwao) kabla ya kusafiri nje. Timu yao ya taifa
inaitwa Red Sea Boys, yaani vijana wa Bahari Nyekundu na haina cha kujivunia
kwenye mashindano haya, ikiwa ilicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa Juni
26, mwaka 1992 na kutoka 1-1 na Sudan.
VIWANGO VYA UBORA FIFA
NCHI NAFASI
Uganda 86
Malawi 101
Ethiopia 102
Sudan 102
Rwanda 122
Burundi 128
Kenya 130
Tanzania 134
Zanzibar 134
Somalia 193
Eritrea 192
Sudan
Kusini 200
(Viwango hivi
vimetoka mwezi huu)