Umony |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
MSHAMBULIAJI
wa Uganda, Brian Umony amesema kwamba yuko tayari sasa kuchezea Tanzania
kuchezea klabu ya Simba ya Dar es Salaam, baada ya kushindikana mwaka 2009,
alipokuwa KCC ya hapa.
Akizungumza
na BIN
ZUBEIRY jana mjini hapa baada ya kuiongoza Uganda kuifunga Sudan Kusini
maao 4-0 katika mechi ya mwisho ya Kundi A, Kombe la Mataifa ya Afrika
Mashariki na kati, CECAFA Tusker Challenge, Umony alisema Simba kama wanamtaka
wamfuate hata sasa wamalizane.
Brian
amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na Express baada ya kumaliza mkataba wake,
Becamex Binh Duong F.C. ya Vietnam.
Mwaka 2009,
baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili
Emmanuel Okwi aliyekuwa Sc Villa wakati huo.
Umony
aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya
Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa
mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C.
Brian
anang’ara katika Kombe la Challenge, hadi sasa ana mabao matatu sawa na
Suleiman Ndikumana wa Burundi na wao ndio wanaongoza kwa mabao, wakifuatiwa na
John Bocco, Khamis Mcha, Chris Nduwarugira, David Ochieng na Clifton Miheso
wenye mabao mawili kila mmoja.
Wengine
wenye bao moja kila mmoja ni Yussuf Ndikumana, Mohamed Jabril, Geoffrey Kizito,
Hamisi Kiiza, Robert Ssentongo, Yonatal Teklemariam, Haruna Niyonzima, Jean
Mugiraneza, Dadi Birori, Ramadhan Salim, Gatech Panom Yietch Ethiopia, Farid
Mohamed, Chiukepo Msowoya, Miciam Mhone, Patrick Masanjala, Amir Hamad Omary na
Yosief Ghide.
Jumla ya
mabao 32 hadi sasa yamefungwa katika mechi 20 za makundi yote matatu,
zilizopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
Suleiman
Ndikumana Burundi 3 (1 penalti)
Brian Umony Uganda 3
John Bocco Tanzania 2
Khamis Mcha Zanzibar 2
Chris
Nduwarugira Burundi 2
David
Ochieng Kenya 2
Clifton
Miheso Kenya 2
Yussuf
Ndikumana Burundi 1
Mohamed
Jabril Somalia 1(penalti).
Geoffrey
Kizito Uganda 1
Hamisi Kiiza Uganda 1
Robert
Ssentongo Uganda 1
Yonatal
Teklemariam Ethiopia 1
Haruna
Niyonzima Rwanda 1
Jean
Mugiraneza Rwanda 1
Dadi Birori Rwanda 1
Ramadhan
Salim Kenya 1
Gatech Panom
Yietch Ethiopia 1
Farid
Mohamed Sudan 1
Chiukepo
Msowoya Malawi 1
Miciam Mhone Malawi 1
Patrick
Masanjala Malawi 1
Amir Hamad
Omary Eritrea 1
Yosief Ghide Eritrea 1(penalti).