// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); UGANDA YAIPA KIPIGO CHA MWANA UKOME SUDAN KUSINI NA KUIRUDISHA NYTUMBANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE UGANDA YAIPA KIPIGO CHA MWANA UKOME SUDAN KUSINI NA KUIRUDISHA NYTUMBANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, November 30, 2012

    UGANDA YAIPA KIPIGO CHA MWANA UKOME SUDAN KUSINI NA KUIRUDISHA NYTUMBANI

    Ssentongo akimtoka beki wa Sudan Kusini

     Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
    UGANDA wamefuzu kwa asilimia 100 hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge baada ya kushinda mechi zake zote za Kundi A, ikiwemo ya leo waliyoshinda 4-0 dhidi ya Sudan Kusini.
    Hakuna mjadala, Sudan Kusini inaondoka katika mashindano haya, bila kuingiza hata pointi moja, wakifungwa mechi zote tatu.
    Uganda na Kenya wamefuzu moja kwa moja, wakati Ethiopia walioshika nafasi ya tatu watasubiri hatima yao kufuzu kama mmoja wa washindi wa watatu bora kutoka makundi yote, A, B na C.
    Katika mchezo wa leo, mabao ya Uganda ambao pia ni mabingwa watetezi yalifungwa na  Brian Umony mawili katika dakika za 23 na 39, Robert Ssentongo dakika ya 47 na Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 79.
    Katika mechi ya kwanza, Kenya ilishinda 3-1 dhidi ya Ethiopia, mabao ya Ramadhan Mohamed Salim, Clifton Miheso na David Ochieng, wakati la Ethiopia lilifungwa na Gatech Panom Yietch.
    Michuano hiyo, itaendelea kesho kwa mechi za Kundi B na C, saa 8:00 mchana, Tanzania Bara watamenyana na Somalia Uwanja wa Lugogo na baadaye saa 10:00, Rwanda itacheza na Eritrea wakati Sudan itaanza na Burundi saa 8:00 mchana Uwanja wa Wankulunkulu na baadaye saa 10:00 jioni Malawi watamenyana na Zanzibar Wankulunkulu.
    Kikosi cha Uganda kilikuwa; Ali Kimera, Robert Ssentongo, Joseph Ochaya, Kweyune Said, Henry Kalungi, Isaac isinde, Manco Kaweesa/Joseph Mpande, Geoffrey Kizito, Nico Wakiro Wadada, Brian Umony/Brian Majwega na Hamisi Kiiza.  

    MSIMAMO KUNDI A:
                          P   W  D   L    GF GA GD Pts
    Uganda          3    3    0    0    6    0    6    9
    Kenya             3    2    0    1    4    2    2    6
    Ethiopia          3    1    0    2    2    3    -1  3
    Sudan Kusini  3    0    0    3    0    7    -7  0

    Beki wa Sudan Kusini akimpitia kwanja kiungo wa Uganda, Joseph Ochaya

    Mashabiki wa Uganda kwa raha zao

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: UGANDA YAIPA KIPIGO CHA MWANA UKOME SUDAN KUSINI NA KUIRUDISHA NYTUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top