UBAKHILI KUWAKOSESHA ARSENAL BONGE LA KIFAA, TENA KINDA TU
Arsenal imetenga dau la pauni Milioni 9 kwa ajili ya winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha, mwenye umri wa mikaka 19 ifikapo Januari, ingawa Mwenyekiti wa klabu yake ya Daraja la Kwanza, Steve Parish amesema mshambuliaji huyo mzaliwa wa Ivory Coast atauzwa kwa pauni Milioni 20.
Manchester City imempa ofa ya majaribio kiungo Hideki Ishige, mwenye umri wa miaka 18, ambaye kwa sasa ni Mwanasoka Bora Chipukizi wa Mwaka Bara la Asia.
CHAMBERLAIN KUWAKOSA MAN U LEO
NYOTA wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain, ataikosa mechi ya leo dhidi ya Manchester United, baada ya kinda huyo wa miaka 19 kuumia tena na kurudi katika 'wadi' ya majeruhi ya Gunners.
Sir Alex Ferguson amesema Manchester United ilikaribia kumsaini Robin van Persie, ambaye leo anajiandaa kupambana na klabu yake ya zamani, Arsenal kwenye Uwanja wa Old Trafford, .
Chanzo cha habari cha karibu na winga wa Manchester United, Nani, mwenye umri wa miaka 25, kimesema kwamba mchezaji huyo alibishana na kocha Alex Ferguson baada ya timu kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Capital One dhidi ya Chelsea Jumatano .
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, mwenye umri wa miaka 34, amesema kwamba bado anaiwaza klabu hiyo ya London, ingawa anafurahia maisha na ushindani wa China.
SHUJAA wa zamani wa Liverpool, Steve Nicol, mwenye umri wa miaka 50, amesema kwamba klabu yake ya zamani lazima isahau kabisa kumsajili winga wa Arsenal, Theo Walcott na kuelekeza fikra zao katika kusajili mfungaji wa uhakika wa mabao.
Alan Shearer, ambaye amekuwa akitazamiwa kupewa kibarua cha ukocha wa Blackburn na Ipswich, hawezi kuhukumiwa tu kwa sababu Newcastle ilishuka Daraja mikononi mwake, kwa mujibu wa Nahodha wa zamani wa Magpies, Rob Lee.
WINGA TELEZA GINOLA AWA KOCHA
Winga wa zamani wa Tottenham na Newcastle, David Ginola, mwenye umri wa miaka 45, amesema kwamba atajiunga na klabu ya Halifax iwapo ataamua kuwa kocha. Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, amemaliza kusoma kozi ya ukocha huko Wales.