Tenga |
Na Princess Asia
RAIS wa
Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Leodger Tenga amewataka wachezaji wa timu
hiyo kuachana na fikra ya kuwa wapinzania wao, Congo Brazaville inaundwa na
wachezaji waliozidi umri ‘Vijeba’ , badala yake vijana hao wajitume ili ushindi
upatikane.
Hatua hiyo
inafuatia kuwepo kwa malalamiko ya Congo Brazavile kuchezesha Vijeba katika
mechi yao ya awali ya kuwania kucheza fainali za Afrika wiki iliyopita jijini
Dar es Salaam ambapo Serengeti ilishinda bao 1-0.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Tenga alisema haoni sababu ya kuwakatia rufaa kama
ilivyoelezwa awali, kwani tayari walisharipoti kwa kamishna wa mchezo huo
na kama watafanya hivyo itakuwa baadaye.
Alisema
wachezaji hao hawana budi kuelekeza akili zao kwenye mechi ya marudiano itakayopigwa
ugenini mwishoni mwa wiki hii na kuhakikisha wanashinda ili kusonga mbele.
“Nisingependa hili neno la Vijeba liingie
katika akili za hawa watoto ili waende kupambana na kurudi na ushind,”alisema.
Aidha, Tenga
amewapongeza vijana hao kwa ushindi walioupata katika mchezo wao wa awali licha
ya kuwa ni finyu na kuwataka kuendelea na moyo wa kujituma ili waweze kufika
mbali.
“Pia TFF inashukuru mashabiki waliojitokeza
kwa wingi kuja kuishangilia timu yao, sambamba na kamati ya kuisaidia Serengeti
kwa mchango wao wa hali na mali,”alisema.
Katika hatua
nyingine, Tenga ametolea ufafanuzi suala la mgawo wa sh mil 1 kati ya mil 23
zilizopatikana katika mchezo wa Serengeti Boys na wenzao wa Congo Brazaville
baada ya kamati ya kuisaidia Serengeti ambayo ilichanga milioni 35 kulalamika.
Tenga
alisema mil.35 zilizochangwa na kamati hiyo zilitumika kufidia hasara
iliyopatikana katika mchezo huo kwani mchezo unaofanyika katika uwanja wa Taifa
na kuingiza chini ya mil.80 ni lazima TFF ibaki na madeni.
“Ndiyo maana tumekuwa tuklipeleka mechi
bndogondogo na zile za vijana katika uwanja wa Uhuru kwa sababu ya gharama za
Uwanja wa Taifa, lakini kutokana na uwanja wa Uhuru kutotumika ndo hatuna dudi
kubaki Taifa na matokeo yake ndiyo kama hivyo.”alisema Tenga.
Tenga
aliongeza kwamba, mara nyingi TFF imekuwa ikipata mzigo wa kulipa madeni
yanayotokana na hasara za michezo mbalimbali inayofanyika kwenye uwanja wa
Taifa.
Tenga
alisema kwa sasa timu hiyo inatakiwa kuendelea kujengwa kisaikolojia ili iweze
kuwa katika hali nzuri na kufanikisha malengo yake ambayo ni muhimu kwa
maendeleo ya soka la Tanzania.
Kikosi cha
wachezaji 18 na viongozi saba wa Serengeti
Boys kinatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Congo Brazzavile tayari
kwa mchezo huo.