Na Princess Asia
SHIRIKISHO
la soka Tanzania (TFF) linaamini kutumika kwa tiketi za kielektroniki katika
mechi mbalimbali nchini utakuwa ni muarobaini wa tatizo la mapato.
Benki ya
CRDB ndiyo imepewa tenda ya kutayarisha tiketi hizo ambazo zitaanza kutunmika
rasmi katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom mwezi Februari mwakani.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Rais wa TFF Leodger Tenga alisema kwamba hatua
hiyo ni jambo la heri na muhimu sana katika kipindi hiki ambacho wadau wamekuwa
wakilalamikia suala la upatikanaji wa mapato kiduchu.
Alisema
pamoja na uzuri wa jambo hilo, lakini wengi watashtuka na kutaka kurudisha
nyuma mchakato huo utakaojenga heshima, lakini Shirikisho hilo halitakubali
kurudishwa nyuma.
“Najua wengi litawaathiri sana kwa namna moja
ama nyingine na hivyo kuanza kuleta vikwazo ili lisifanikiwe, tumesimama imara
kuhakikisha hili linatimia ili kujenga heshima,”alisema Tenga