Musonye |
Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
TELEVISHENI ya kulipia ya kimataifa, SuperSport ya Afrika
Kusini inarusha mashindano ya Kombe la mataifa ya Afrika Mashariki, CECAFA
Tusker Challenge bila kulipia chochote, imeelezwa.
Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA), Nicholas Musonye ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, wameamua
kuwapa haki ya kurusha matangazo SuperSport bila malipo, ili kuitangaza soka ya
ukanda huu.
“Watu wamekuwa wakilalamika sana kwamba mashindano ya CECAFA
hayaonekani kwenye TV, sasa sisi tukaamua kuwapa haki hiyo bure SuperSport ili
kupromoti soka yetu, je ni vibaya?”alihoji Musonye.
Pamoja na SuperSport kurusha matangazo hayo bure, Musonye
ameondoa dhana kwamba, Televisheni nyingine za nchi za CECAFA zinazuiwa kurusha
matangazo hayo.
“Hakuna TV ambayo inazuiwa, Tanzania TBC huwa wanaonyesham
Kenya KBC huwa wanaonyesha na Uganda pia UBC wanaonyesha, hatuzuii sisi TV
kurusha matangazo yetu,”alisema Musonye.
Wakati SuperSport ikirusha bure matangazo ya mashindano ya
CECAFA, nchini Tanzania Kamati ya Ligi Kuu inazuia Vituo vya Redio na
Televisheni kurusha bure mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na hivi
sasa kuna mgogoro mkubwa baina ya pande hizo mbili.