Kikosi cha Stars |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
MICHUANO ya Kombe
la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge inatarajiwa
kufikia tamati leo kwa hatua yake ya makudi, kwa mechi nne za Kundi B na C
kupigwa kwenye viwanja tofauti mjini hapa.
Tanzania
Bara, Kilimanjaro Stars watamenyana na Somalia kuanzia saa 8:00 mchana, kwenye Uwanja
wa Lugogo na baadaye saa 10:00, Rwanda itacheza na Eritrea kwenye Uwanja huo
huo.
Sudan itamenyana
na na Burundi kuanzia saa 8:00 mchana kwenye Uwanja wa Wankulunkulu na baadaye
saa 10:00 jioni Malawi watamenyana na Zanzibar Wankulunkulu kwenye Uwanja huo
huo.
Mechi hizo, zimehamishwa kutoka Uwanja wa Mandela, Namboole,
kutokana na Uwanja huo kuharibika na mvua zilizofululiza mjini na hapa na
CECAFA imeamua kuupumzisha kwa muda.
Kocha wa
Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen amefurahia kupona kwa beki Shomary Kapombe na
ana matumaini ya kumtumia leo, ingawa kiungo Mwinyi Kazimoto ataendelea
kujiuguza.
Daktari wa Stars,
Dk Mwanandi Mwankemwa, amesema mchezaji Kazimoto hataweza kucheza kwa kuwa bado
anaendelea kupata nafuu kwa hivyo wamemshauri kocha ampumzishe katika mechi ya
kesho.
Stars pia
itamkosa beki wake wa kushoto chaguo la kwanza, Amir Maftah ambaye ana kadi
mbili za njano.
Kocha huyo
Mdenmark, amesema kwamba mechi ya leo itakuwa ni ya kufa na kupona na kikosi
chake kiko tayari kukamilisha kazi.
“Mechi hii
ni sawa na kuwa na risasi moja na risasi hii unatakiwa kuitumia vizuri..ndio
mtihani tunaokabiliwa nao katika mechi hii maana lazima tushinde ili tusinonge
mbele katika mashindano haya,” alisema n akikosi chake kitapambana hadi dakika
ya mwisho.
Alisema ana
imani na kikosi chake kwani wachezaji wote wana ari ya ushindi na kuendelea na
mashindano kwani wameshaonesha kiwango kikubwa katika mechi mbili zilizopita
huku Stars ikishinda mechi moja shidi ya Sudan na kufungwa nyingine na Burundi.
“Katika
mechi hii hakuna mchezo na nimeshawaambia wachezaji kabisa maana hapa ukifungwa
unaondoka,” alisema.
Meneja wa
Bia ya Kilimanajro Premium Lager, wadhamini wa Stars, George Kavishe ametuma
salamu muhimu hapa Kampala akisema kwamba mechi hii ni muhimu kwa Stars na
kuwaomba Watanzania wanaoishi Uganda kujitokeza kwa wingi kuishangilia.
“Vijana hawa
wanahitaji sapoti kutoka kwa wadau wote
hasa katika mechi hii ya kesho itakayoamua kama Tanzania itafuzuu
kuendelea au la….sisi tukiwa wadhamini wa timu tunafuatilia kwa karibu na
tunawaomba Tanzania waishangilie na kuipa moyo timu yao,” alisema.
Kikosi cha
Stars kinachotarajiwa kuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari
Kapombe, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba, John Bocco,
Shaaban Nditi na Salum Abubakar.
MSIMAMO
KUNDI A:
P W D L GF GA GD Pts
Uganda 3 3 0 0 6 0 6 9
Kenya 3 2 0 1 4 2 2 6
Ethiopia 3 1 0 2 2 3 -1 3
Sudan Kusini 3 0 0 3 0 7 -7 0
MSIMAMO
KUNDI B:
P W D L GF GA GD Pts
Burundi 2 2 0 0 6 1 5 6
Tanzania 2 1 0 1 2 1 1 3
Sudan 2 1 0 1 1 2 -1 3
Somalia 2 0 0 2 1 6 -5 0
MSIMAMO
KUNDI C:
P W D L GF GA GD Pts
Zanzibar 2 1 1 0 2 1 1 4
Rwanda 2 1 0 1 3 2 1 3
Malawi 2 1 0 1 3 4 -1 3
Eritrea 2 0 1 1 2 3 -1 1
VIWANGO VYA
UBORA FIFA
NCHI NAFASI
Uganda 86
Malawi 101
Ethiopia 102
Sudan 102
Rwanda 122
Burundi 128
Kenya 130
Tanzania 134
Zanzibar 134
Somalia 193
Eritrea 192
Sudan Kusini 200
(Viwango hivi vimetoka mwezi huu)