// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); STARS WALALAMIKIA UWANJA MBOVU WA MAZOEZI KAMPALA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE STARS WALALAMIKIA UWANJA MBOVU WA MAZOEZI KAMPALA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, November 24, 2012

    STARS WALALAMIKIA UWANJA MBOVU WA MAZOEZI KAMPALA

    Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Edward Christopher akikokota mpira wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara nchini Uganda leo kujianda na mchezo wa kesho dhidi ya Sudan Kundi B, michuono ya Tusker Challenge. 
    Kevin Yondan aliyeipa mgongo kamera (5) akitaniana na wenzake baada ya mazoezi leo

     Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
    TIMU ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars imelalamikia Uwanja mbovu wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara, waliopelekwa kufanya mazoezi leo kujiandaa na mechi ya kesho ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge 2012 dhidi ya Sudan, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura amewasilisha malalamiko hayo kwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Rodgers Mulindwa ambaye ameahidi kuyafanyia kazi.
    “Tutalifanyia kazi suala hilo, tutakuwa na kikao kesho litawasilishwa na litapatiwa usumbufu, mwanzo huwa na matatizo, lakini mambo yatakuwa mazuri,”alisema Mulindwa.
    Hata hivyo, inashangaza Stars kupelekwa katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara, wakati kwenye mpango wa awali kabisa wa FUFA ilitakiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Nakawa.    
    Kwa upande wake, kocha wa Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesikitishwa na kutowasili kwa washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    “Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaweza wasicheze katika mechi ya kesho kwa sababu hawajafika, lakini mimi nikiwa kocha nimejiandaa vizuri na nina imani na wachezaji waliopo,” alisema.
    “Nina imani TFF wanafuatilia suala hili na wachezaji hawa watajiunga na wenzao hivi karibuni lakini hii haituzuii kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri,” alisema.
    Alisema wachezaji wote wana hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Sudan ambazi zimo katika Kundi B pamoja na Burundi na Somalia ambazo zitacheza leo pia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: STARS WALALAMIKIA UWANJA MBOVU WA MAZOEZI KAMPALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top