Kikosi cha Taifa Stars kilichoifunga Gambia 2-1 |
Na Prince Akbar
KIKOSI cha
timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimeingia kambini leo mjini
Mwanza kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kenya, Harambee
Stars Jumatano, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Wachezaji walioitwa
kwenye timu hiyo ni makipa Juma Kaseja (Simba SC) na Deogratius Mushi ‘Dida’ wa
Azam FC.
Mabeki;
Kevin Yondan (Yanga), Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam FC), Issa Rashid (Mtibwa
Sugar), Nassoro Masoud ‘Cholo’, Shomari Kapombe na Amir Maftah (Simba).
Viungo; Salum
Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Singano ‘Messi’
na Mrisho Ngassa (Simba), Athuman Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo (Yanga) na Shaaban
Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji;
John Bocco ‘Adebayor’ (Azam FC), Simon Msuva (Yanga), Christopher Edward (Simba),
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa (TPM, DRC).
Wachezaji wote
hao tayari wapo kambini katika hoteli ya La Kairo, maeneo ya Kirumba na leo
wamefanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini humo tayari kwa mchezo huo
ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).