Mwinyi Kazimoto, mmoja wa wachezaji wanaoiwakilisha Simba katika Tusker Challenge 2012 |
Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
MABINGWA wa
Tanzania Bara, Simba SC wanaongoza kuwa na wachezaji wengi katika Mashindano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na kati, Tusker Challenge 2012 inayoanza
leo mjini hapa, wakiwa na jumla ya wachezaji 10, yaani kasoro mmoja tu kuunda kikosi
kamili cha kwanza.
Wachezaji wa
Simba waliopo hapa na timu zao kwenye mabano ni Nassor Masoud 'Cholo'
(Zanzibar), Juma Kaseja (Bara), Shomari Kapombe (Bara), Amir Maftah (Bara),
Amri Kiemba, (Bara) Mwinyi Kazimoto (Bara), Ramadhani Singano ‘Messi’ (Bara),
Mrisho Ngassa (Bara), Christopher Edward (Bara) na Emanuel Okwi (Uganda).
Simba wenye
maskani yao pale Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam wanafuatiwa na Azam FC ya
Chamazi, kuwa na idadi kubwa ya wachezaji kwenye mashindano haya yanayofunguliwa
leo na rais wa Shirkisho la Soa Afrika (CAF), Issa Hayatou Uwanja wa Mandela,
uliopo Namboole, Kampala.
Wachezaji wa Simba na timu zao kwenye mabano ni Nassor Masoud 'Cholo' (Zanzibar), Juma Kaseja
(Bara), Shomari Kapombe (Bara) na Amir Maftah (Bara), Amri Kiemba, (Bara) Mwinyi
Kazimoto (Bara), Ramadhan Singano ‘Messi’ (Bara), Mrisho Ngassa (Bara),
Christopher Edward (Bara) na Emanuel Okwi (Uganda).
Wachezaji wa
Azam waliopo hapa na timu zao kwenye mabano ni Mwadini Ali (Zanzibar), Samir
Haji Nuhu (Zanzibar), Aggrey Morris (Zanzibar), Abdulhalim Humud (Zanzibar),
Khamis Mcha 'Vialli' (Zanzibar) ,Deogratius Munishi ‘Dida’ (Bara), Erasto
Nyoni (Bara), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Bara) na John Bocco ‘Adebayor’ (Bara).
Azam yenye
wachezaji tisa, inafuatiwa na mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Yanga SC
wenye wachezaji wanane, wakati klabu nyingin za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara zenye wachezaji Challenge ni Mtibwa Sugar ya Morogoro watatu, JKT Oljoro
ya Arusha mmoja sawa na Coastal Union ya Tanga.
Yanga
inawakilishwa na Nadir Haroub Ali 'Canavaro'(Zanzibar), Didier Kavumbangu
(Burundi), Haruna Niyonzima (Rwanda), Hamisi Kiiza (Uganda), Kevin
Yondan (Bara), Athuman Iddi ‘Chuji’ (Bara), Frank Domayo (Bara) na Simon Msuva (Bara),
wakati Mtibwa Sugar ni Twaha
Mohammed (Zanzibar), Issa Rashid (Bara) na Shaaban Nditi (Bara).
Maafande wa
Jeshi la Kujenga Taifa kutoka Arusha, JKT Oljoro wao wanawakilishwa na Amir
Hamad aliye na kikosi cha Zanzibar, wakati Wagosi wa Kaya, Coastal Union wanawakilishwa
na Suleiman Kassim 'Selembe' aliye na Zanzibar pia.
LIGI KUU BARA INAVYOWAKILKISHWA
CHALLENGE:
Simba (10); Nassor Masoud 'Cholo' (Zanzibar), Juma Kaseja
(Bara), Shomari Kapombe (Bara) na Amir Maftah (Bara), Amri Kiemba, (Bara) Mwinyi
Kazimoto (Bara), Ramadhan Singano ‘Messi’ (Bara), Mrisho Ngassa (Bara),
Christopher Edward (Bara) na Emanuel Okwi (Uganda).
Azam (9); Mwadini Ali (Zanzibar), Salmin Haji
Nuhu(Zanzibar), Agrey Moris(Zanzibar), Abdulhalim Humoud(Zanzibar), Khamis Mcha
Khamis 'Viali'(Zanzibar) ,Deogratius Mushi ‘Dida’ (Bara), Erasto Nyoni (Bara),
Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Bara), John Bocco ‘Adebayor’ (Bara).
Yanga (8); Nadir Haroub Ali 'Canavaro'(Zanzibar),
Didier Kavumbangu (Burundi), Haruna Niyonzima (Rwanda), Hamisi Kiiza (Uganda), Kevin Yondan
(Bara), Athuman Iddi ‘Chuji’ (Bara), Frank Domayo (Bara), Simon Msuva (Bara).
Mtibwa Sugar(3); Twaha Mohammed (Zanzibar), Issa Rashid
(Bara), Shaaban Nditi (Bara)
JKT oljoro(1); Amir Hamad (Zanzibar)
Coastal Union(1); Suleiman Kassim 'Selembe' (Zanzibar)