Farid Mussa Shah wa Serengeto kulia akichuana na beki wa Kongo Brazzaville Tmouele Ngampio katika mechi hiyo |
Na Princess Asia
MECHI ya
mchujo ya Kombe la Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya
Tanzania, Serengeti Boys na Kongo Brazzaville iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam imeingiza Sh. 23,021,000.
Ofisa Habari
wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mapato hayo
yametokana na washabiki 18,022 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa
viingilio vya sh. 10,000, sh. 5,000, sh. 2,000 na sh. 1,000. Washabiki 15,850
walikata tiketi za sh. 1,000.
Amesema asilimia
18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 3,511,677.97 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko
la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 5,956,635),
usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh.
400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000), umeme (sh. 300,000) na
ulinzi wa mechi (sh. 3,500,000).
Kwa upande wa
mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 1,000,537, asilimia 10 ya uwanja
sh. 500,269, asilimia 5 ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) sh. 250,134,
asilimia 45 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,251,209,
asilimia 20 ya TFF (sh. 1,000,537) na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) sh.
50,027.