Ndikumana |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
MSHAMBULIAJI
wa zamani wa Simba SC, Suleiman Yamin Ndikumana kwa sasa ndiye anaongoza kwa
kufunga mabao katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati,
CECAFA Tusker Challenge inayoendelea mjini hapa.
Ndikumana
aliyewahi pia kucheza Norway na Uturuki, jana alifunga bao la tatu katika
mashindano haya, akiichezea Burundi dhidi ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars.
Sasa
anamzidi kwa bao moja, John Bocco ‘Adebayor’ wa Kilimanjafo Stars.
Jumla ya
mabao 17 hadi sasa yamefungwa katika mechi 16 za makundi yote matatu,
zilizopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala.
Bocco anafungana
na mshambuliaji mwingine wa Burundi, Christopher Nduwarugira, wakati wachezaji
wengine ambao hadi sasa kila mmoja amefunga bao moja ni Farid Mohamed, Yussuf
Ndikumana wa Burundi, Mohamed Jabril wa Somalia kwa penalti, Geoffrey Kizito wa Uganda, Yonatal Kebede Teklemariam, Haruna
NiyonzimUganda, David Ochieng, Clifton Miheso na Jean Mugiraneza.
Kwa sasa
Bocco anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, ndiye mshambuliaji pekee kwenye
kikosi cha Bara, baada ya washambuliaji wengine, Mbwana Samatta na Thomas
Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemomkrasia ya Kongo (DRC)
kuzuiliwa na klabu yao.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
Suleiman
Ndikumana Burundi 3 (1 penalti)
John Bocco Tanzania 2
Chris
Nduwarugira Burundi 2
Yussuf
Ndikumana Burundi 1
Mohamed
Jabril Somalia 1(penalti).
Geoffrey
Kizito Uganda 1
Brian Umony Uganda 1
Yonatal
Teklemariam Ethiopia 1
Haruna
Niyonzima Rwanda 1
Jean
Mugiraneza Rwanda 1
David
Ochieng Kenya 1
Clifton
Miheso Kenya 1
Farid
Mohamed Sudan 1