MWIMBAJI nyota wa miondoko ya Taarab, Mariam Khamis “Paka Mapepe” amefariki alfajiri ya leo katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili.
Mariam Khamis ambaye hadi anafariki alikuwa ni mwajiriwa wa TOT Taarab alipelekwa Muhimbili kwa ajili ya uzazi na inasemekana mtoto ametoka salama lakini yeye Mungu amempenda zaidii.
Mtu wa karibu sana na mwimbaji huyo, Thabit Abdul ameithibitishiawww.saluti5.com kuwa ni kweli Mariam Khamis amefariki dunia.
Aidha mwimbaji Isha Ramadhan “Mashauzi” naye akiongea na saluti5 kutoka Muhimbili nae alithibitisha kutokea kwa kifo hicho “Ni kweli Mariam amefariki na hivi tunavyoongea tayari tupo hapa Muhimbili” Alisema Isha.
Mariam Khamis alitamba sana na wimbo wa Mapaka Mapepe alouimba akiwa na Melody, kabla ya kujiunga na Zanzibar Stars, Five Stars na hatimae TOT.
Wimbo wake wa kwanza kurekodi na TOT ni Sidhuriki na lawama ambao unatamba sana hadi leo hii