Athimani Iddi 'Chuji' wa Yanga kulia akiwa katika moja ya mechi za Ligi Kuu dhidi ya Mgambo JKT. Je, ataingia kwenye orodha ya wachezaji wa kuwanai tuzo ya Mwanasoka Bora Tanzania? |
Na Prince Akbar
FAINALI ya
tuzo za Mwanasoka Bora wa mwaka Tanzania, zinazotolewa na Kampuni ya Wazalendo
Bright Media zinatarajiwa kufanyika Desemba 30 mwaka huu mjini Dar es Salaam
katika sehemu, ambayo itatangazwa baadaye.
Mratibu wa
mchakato huo, Ahadi Kakore ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mchakato wake
ulianza tangu Agosti mosi mwaka huu kwa wanamichezo kupigiwa kura na mashabiki
kupitia mitandao mbalimbali ikiwemo ile ya kijamii (face book, Twitter na
Blogs) na wengine kwa njia ya simu za mikononi kwa kupitia namba maalum.
Amesema kwa
sasa kamati ipo kwenye mchakato ya kuchuja majina ambayo yamependekezwa na mashabiki wa soka kupitia kura zao ambapo
zaidi ya wachezaji 93 wanaocheza Ligi Kuu Tanzania Bara majina yao yameweza
kuonekana ambapo kati ya majina hayo yataopunguzwa na kufikia 30.
Amesema kabla
ya kufanyika kwa fainali hiyo wale wachezaji ambao wataingia kwenye fainali
watapatiwa semina ya uwezekezaji na ujasiriamali ili kujiandaa na maisha ya
baadaye baada ya kustaafu.
Amesema sababu
za kufanya semina hii ni kuhakikisha kuwa wachezaji wetu wanapata elimu ya
uwezekaji na ujasiriamali ili kuwekeza kwenye sekta mbalimbali kwa ajili ya
siku zijazo hasa ikizingatiwa kwamba wachezaji wengi wa Tanzania bado ni
masikini.
Kakore amesema
kwenye semina hiyo watakuwepo wataalam waliobobea kwenye mambo ya uchumi na
fedha ambao watatoa elimu ya uwekezaji, kwa kufanya hivi itawapa nafasi
wachezaji hawa kuelewa na kutambua umuhimu wa uwekezaji.
Amesema semina
hiyo inatarajiwa kufanyika Desemba 19 na
20 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.
Pamoja semina ambayo itakwenda sambamba na
utoaji wa elimu ya afya kwa washiriki wa semina hiyo ambao watakuwa
wachezaji pekee. Amesema mshindi wa tunzo hiyo anatarajiwa kupata tuzo, fedha
taslim, medali na cheti.