Katibu wa
Yanga, Lawrence Mwalusako amesahihisha taarifa alizotoa jana kuhusu uteuzi wa
Meneja mpya wa timu na Ofisa Habari. Mwalusako amesema Shaaban Katwila
aliyemtaja jana kuajiriwa kama Meneja mpya wa timu na Bakari Kizuguto
aliyetajwa kuwa Ofisa Habari, kwa usahihi wameomba tu kazi, lakini
hawajapitishwa katika ajira bado. Mwalusako ameomba radhi wapenzi wa soka,
hususan wanachama na mashabiki wa Yanga kwa usumbufu wowote uliojitokeza
kutokana na taarifa hizo. Amesema mchakato wa kuwapata Maofisa wapya wa kushika
nyadhifa hizo bado unaendelea.
Pichani
ni Mwalusako (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu,
makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Kariakoo, Dar es Salaam leo kusahihisha
taarifa yake ya jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa klabu hiyo. |