John Bocco kushoto |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
KATIKA mechi
sita za awali za makundi yote kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika
Mashariki, CECAFA Tusker Challenge hadi jana jumla ya mabao 12 yamefungwa.
Baada ya
kila timu kushuka dimbani mara moja, Burundi ndiyo wameweza kuvuna mabao mengi
katika mechi moja, matano wakifuatiwa na Tanzania Bara na Rwanda, waliovuna
mabao mawili kila mmoja.
Mshambuliaji
wa Tanzania John Bocco anachuana kwa ufungaji na washambuliaji wa Burundi, Chris
Nduwarugira na Suleiman Ndikumana, ambao kila mmoja ana mabao mawili pia.
Wengine
ambao hadi sasa kila mmoja amefunga bao moja ni Yussuf Ndikumana wa Burundi, Mohamed
Jabril wa Somalia kwa penalti, Geoffrey
Kizito wa Uganda, Yonatal Kebede Teklemariam, Haruna Niyonzima na Jean
Mugiraneza.
Bocco ana
nafasi zaidi ya kuongeza mabao katika mechi za kundi hilo, haswa kwenye mchezo
dhidi ya Somalia Desemba 1, kwani hiyo ndio timu dhaifu zaidi kwenye Kundi B.
Lakini Bocco
kama atacheza kwa kiwango cha jana, anaweza akawa mwiba hata mbele ya Burundi Novemba 28.
Kwa sasa
Bocco anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, ndiye mshambuliaji pekee kwenye
kikosi cha Bara, baada ya washambuliaji wengine, Mbwana Samatta na Thomas
Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemomkrasia ya Kongo (DRC)
kuzuiliwa na klabu yao.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
John Bocco Tanzania 2
Yussuf
Ndikumana Burundi 2
Suleiman
Ndikumana Burundi 2
Yussuf
Ndikumana Burundi 1
Mohamed
Jabril Somalia 1(penalti).
Geoffrey
Kizito Uganda 1
Yonatal
Teklemariam Ethiopia 1
Haruna
Niyonzima Rwanda 1
Jean
Mugiraneza Rwanda 1