// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MASHABIKI KANDA YA ZIWA WAENDA KUISAPOTI STARS KAMPALA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MASHABIKI KANDA YA ZIWA WAENDA KUISAPOTI STARS KAMPALA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, November 23, 2012

    MASHABIKI KANDA YA ZIWA WAENDA KUISAPOTI STARS KAMPALA

    
    Frank Domayo, kiungo wa Kili Stars
    
    Na Mahmoud Zubeiry
    UMOJA wa wanamichezo waliowahi kucheza klabu mbalimbali zikiwemo za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara wenye maskani yao mjini Bukoba, Kagera, Bukoba Veteran Sports Club ni katika kuhamasisha ushiriki wa timu za Tanzania, Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes, kwenye michuano ya Kombe la Tusker Challenge inayofanyika jijini Kampala Uganda, umeandaa safari ya mashabiki walioko mkoani humo Kanda ya Ziwa kwa ujumla kwenda kushangilia mechi za timu hizo.
    Katibu Mkuu wa Bukoba Veterans, Shijja Richard ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba kwa kuanzia, mashabiki hao wataondoka mjini Bukoba Jumapili Novemba 25, 2012 kwenda kuishangilia timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo dhidi ya Sudan Kaskazini.
    Amesema nia na madhumuni ya safari hiyo ni kuhamasisha wachezaji wa timu za taifa za Tanzania waweze kufanya vizuri katika michuano hiyo mikubwa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kutoa hamasa kwa watanzania kujenga tabia ya kushangilia timu zao na pia wanadhani kuwa ushiriki wao utaongeza ushindani katika michuano hiyo.
    Amesema tayari taratibu zote zimeshafanyika ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) ili wawasiliane na mamlaka zinazohusika kwa ajili ya kupatiwa eneo maalumu uwanjani litakalowezesha watanzania waweze kuishangilia vizuri timu ya taifa.
    “Tunatarajia kwenda uwanjani na zaidi ya mashabiki 60 ambao hivi sasa wanakamilisha taratibu za mwisho za kuvuka mpaka wa nchi. Matarajio yetu ni kuendelea kuziunga mkono timu za taifa katika michuano hiyo hadi kufikia mwisho wa michuano. Tunaomba watanzania wengine walioko kanda ya ziwa katika mikoa ya Shinyanga, Mara na Mwanza watuunge mkono,”alisema Richard.
    Kikosi cha kinatarajiwa kuwasili leo mjini Kampala, kikitokea Mwanza tayari kwa mashindano hayo ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Tusker Challenge 2012 yanayotarajiwa kuanza kesho.
    Stars imekuwa kambini mjini Mwanza kwa takriban wiki mbili sasa ikijifua vikali chini ya kocha wake, Mdenmark Kim Poulsen kujiandaa kwenda kutwaa taji la nne la Challenge.
    Kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichopo kambini mjini Mwanza, kinaundwa na makipa; Juma Kaseja (Simba SC) na Deogratius Mushi ‘Dida’ wa Azam FC, mabeki; Kevin Yondan (Yanga), Erasto Nyoni (Azam FC), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Shomari Kapombe na Amir Maftah (Simba).
    Viungo ni Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Mrisho Ngassa (Simba), Athuman Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo (Yanga) na Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar) wakati washambuliaji ni John Bocco ‘Adebayor’ (Azam FC), Simon Msuva (Yanga), Christopher Edward (Simba), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa (TPM, DRC).
    Bara ambayo inajivunia kutwaa mara tatu Kombe la Challenge katika miaka ya 1974, 1994 na 2010 na kushika nafasi ya pili mara tano, imepangwa Kundi B pamoja na Sudan, Burundi na Somalia.
    Itaanza kampeni zake Novemba 25 kwa kumenyana na Sudan saa 12:00 jioni, mchezo utakaotanguliwa na mechi kati ya Burundi na Somalia itakayoanza saa 9:00 Alasiri kabla ya kurudi tena dimbani, Novemba 28 kukipiga na Burundi, mchezo utakaotanguliwa na mechi kati ya Somalia na Sudan.
    Stars iatahitimisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na Somalia Desemba 1, mchezo utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Sudan na Burundi. Mechi zote za Stars zitakuwa saa 12:00 jioni.

    MAKUNDI RATIBA TUSKER CHALLENGE 2012:
    KUNDI A: Uganda, Kenya, Ethiopia na Sudan Kusini
    KUNDI B: Tanzania, Sudan, Burundi na Somalia
    KUNDI C: Malawi, Eritrea, Rwanda na Zanzibar

    RATIB KUNDI A:
    Novemba 24, 2012:
    Ethiopia v Sudan                 (Saa 9:00 Alasiri)
    Uganda v Kenya                  (Saa 12:00 jioni)
    Novemba 27, 2012:
    Sudan Kusini v Kenya         (Saa 9:00 Alasiri)
    Uganda v Ethiopia              (Saa 12:00 jioni)
    Novemba 30, 2012:
    Kenya v Ethiopia                 (Saa 9:00 Alasiri)
    Sudan Kusini v Uganda      (Saa 12:00 jioni)

    RATIBA KUNDI B:
    Novemba 25, 2012:
    Burundi v Somalia               (Saa 9:00 Alasiri)
    Tanzania v Sudan                (Saa 12:00 jioni)
    Novemba 28, 2012:
    Somalia v Sudan                  (Saa 9:00 Alasiri)
    Tanzania v Burundi             (Saa 12:00 jioni)
    Desemba 1, 2012:
    Sudan v Burundi                  (Saa 9:00 Alasiri)
    Somalia v Tanzania             (Saa 12:00 jioni)

    RATIBA KUNDI C:
    Novemba 26, 2012:
    Zanzibar v Eritrea         (Saa 9:00 Alasiri)
    Rwanda v Malawi         (Saa 12:00 jioni)
    Novemba 29, 2012:
    Malawi v Eritrea                  (Saa 9:00 Alasiri)
    Rwanda v Zanzibar             (Saa 12:00 jioni)
    Desemba 1, 2012:
    Malawi v Zanzibar               (Saa 9:00 Alasiri)
    Eritrea v Rwanda                 (Saa 12:00 jioni)

    ROBO FAINALI:
    Desemba 3, 2012
    Mshindi Kundi C vs Mshindi wa Pili Kundi B (Saa 10:00 jioni)
    Mshindi Kundi A vs Mshindi wa Tatu Bora wa pili (Saa 1:00 usiku)
    Desemba 4, 2012 (16:00):
    Mshindi Kundi B vs Mshindi wa Tatu Bora wa kwanza (Saa 10:00 jioni)
    Mshindi wa Pili Kundi A vs Mshindi wa Pili Kundi C    (Saa 1:00 usiku)

    NUSU FAINALI:
    Desemba 6, 2012
    Nusu Fainali ya Kwanza     (Saa 10:00 jioni)
    Nusu Fainali ya Pili              (Saa 1:00 usiku)

    MSHINDI WA TATU:
    Desemba 8, 2012
    Waliofungwa Nusu Fanali (Saa 10:00 jioni)

    FAINALI:
    Desemba 8, 2012
    Walioshinda Nusu Fainali  (Saa 1:00 usiku)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MASHABIKI KANDA YA ZIWA WAENDA KUISAPOTI STARS KAMPALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top