John Bocco 'Adebayor' |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
MSHAMBULIAJI
tegemeo wa Tanzania, John Bocco ‘Adebayor’ bado anaongoza kwa mabao katika
michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki, CECAFA Tusker Challenge baada
ya mechi 14 kuchezwa hadi hadi jana.
Jumla ya
mabao 15 hadi sasa yamefungwa katika mechi 14 za makundi yote matatu,
zilizopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala.
Bocco
anachuana kwa ufungaji na washambuliaji wa Burundi, Chris Nduwarugira na
Suleiman Ndikumana, ambao kila mmoja ana mabao mawili pia.
Wengine
ambao hadi sasa kila mmoja amefunga bao moja ni Yussuf Ndikumana wa Burundi, Mohamed
Jabril wa Somalia kwa penalti, Geoffrey
Kizito wa Uganda, Yonatal Kebede Teklemariam, Haruna NiyonzimUganda, David
Ochieng, Clifton Miheso na Jean Mugiraneza.
Bocco ana
nafasi zaidi ya kuongeza mabao katika mechi za kundi hilo, haswa kwenye mchezo
dhidi ya Somalia Desemba 1, kwani hiyo ndio timu dhaifu zaidi kwenye Kundi B.
Lakini Bocco
kama atacheza kwa kiwango cha mechi dhidi ya Sudan, anaweza akawa mwiba hata leo
mbele ya Burundi.
Kwa sasa
Bocco anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, ndiye mshambuliaji pekee kwenye
kikosi cha Bara, baada ya washambuliaji wengine, Mbwana Samatta na Thomas
Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemomkrasia ya Kongo (DRC)
kuzuiliwa na klabu yao.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
John Bocco Tanzania 2
Yussuf
Ndikumana Burundi 2
Suleiman
Ndikumana Burundi 2
Yussuf
Ndikumana Burundi 1
Mohamed
Jabril Somalia 1(penalti).
Geoffrey
Kizito Uganda 1
Brian Umony Uganda 1
Yonatal
Teklemariam Ethiopia 1
Haruna
Niyonzima Rwanda 1
Jean
Mugiraneza Rwanda 1
David
Ochieng Kenya 1
Clifton
Miheso Kenya 1