LIVERPOOL YAMTENGEA DAU WALCOTT
.
Liverpool inafuatilia mustakabali wa mkataba wa Theo Walcottkatika klabu yake, Arsenal na Kocha wa Wekundu hao, Brendan Rodgers anaweza kutumia kiasi cha pauni Milioni 10 kama ada ya uhamisho ya mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 23.
Mpango wa Chelsea kumsajili kiungo Mbrazil mwenye umri wa miaka 24, Paulinho, ambaye pia anatakiwa na Inter Milan, unaweza kubuma kufuatia klabu yake, Corinthians kukanusha mpango wa kumuuza.
Ikiwa imemsajili Jan Vertonghen mwishoni, Tottenham inamtolea macho beki mwingine Mbelgiji anayechezea Ajax, mwenye thamani ya pauni Milioni 8, Toby Alderweireld ambaye ana umri wa miaka 23.
Beki ambaye hana thamani kwa sasa Manchester City, Kolo Toure, mwenye umri wa miaka 31, amesema angependa kuhamia Ufaransa.
West Ham inataka kumsajili kinda wa umri wa miaka 21, mshambuliaji wa Croatia, Andrej Kramaric, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Lokomotiva akitokea Dinamo Zagreb.
MANCINI ALITAKA KWENDA MONACO
Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini ameripotiwa kufanya mazungumzo na Monaco wkwa lengo la kujiunga nao msimu uliopita.
KEANE AITWA SHABIKI MAREKANI
Mshambuliaji wa zamani wa Spurs, Robbie Keane, ambaye kwa sasa anacheza timu moja na David Beckham, LA Galaxy, ametambulishwa kama shabiki asiyetambulika katika maelezo ya picha aliyopigwa akiwa na Beckham na mchekeshaji, Russell Brand.