Na Princess Asia
MWANAMUZIKI
mkongwe nchini, Lady Jadee ameanzisha kipindi cha TV kiitwacho Diary Ya Lady
Jaydee, kitakachokuwa kikirushwa hewani na kituo cha East African TV, maarufu
kama Channel 5 kila Jumapili saa 3:00 usiku.
Kama msanii,
Lady Jaydee amefanikiwa na kutambulika katika kiwanda cha muziki ndani na nje
ya nchi, huku akitunukiwa tunzo nyingi zaidi akiwa albamu zake tano. Pamoja na
kuwa anaendelea na fani yake ya muziki, Lady Jaydee ameamua kuwafikia na
kuwaburudisha wapenzi wa kazi zake kwa njia nyingine.
Lady Jaydee
sasa anaanza sura mpya ya burudani kwa kuleta kipindi cha TV kiitwacho DIARY YA
LADY JAYDEE, ambacho kutaonekana katika kituo cha TV cha EATV
Diary Ya
Lady Jaydee itaonesha maisha na hadithi za kweli za Lady Jaydee kwa lengo la kuburudisha
kwa kuonyesha mambo yate mazuri anayopitia au kuyaona Lady Jaydee kuelimisha
kwa kushiriki mambo ya kijamii, kutia moyo wengine wafuate ndoto zao kwa
uadilifu, kuongeza kipato kama msanii kwa kutangaza biashara mbalimbali na
hatimae kudumisha ajira binafsi kwa njia ya sanaa.
Lady Jaydee
anatoa shukrani kwa mashabiki kwa kuendelea kumpokea, jambo ambalo linampa
nguvu zaidi ya kufanya kaza.
Pia
anashukuru sana vyombo vya habari na zaidi anawashukuru EATV na washirika wake
kwa kumpa nafasi ya kurusha kipndi chake kipya Diary Ya Lady Jaydee. EATV
imekuwa mchango wa aina yake katika kuwakuza wasanii Tanzania.
Lady Jaydee
anatoa wito kwa vyombo vya habari kuendelea kushirikiana na naye kwa kila
namna, ili kukuza na kuendeleza kipaji chake na sanaa ya muziki wa Tanzania kwa
ujumla wake.
Zaidi anatoa
wito kwa makampuni kishiriki na kuungana nae ili waweze kumpa nguvu msanii,
kutangaza biashara zao na kushawishi ajira katika fani ya muziki.
Na mwisho
Lady Jaydee anawaribisha wote kusikiliza CDs zake au kuburidika na kundi lake
la Machozi Band au kupata chakula ktk mgahawa wake wa kisasa Nyumbani Lounge au
ukiwa umepumzika nyumbani utazame kipindi chake Diary Ya Lady Jaydee ktk EATV.