Shangwe hizi zitaendelea kwa Uganda leo? |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
MECHI za Kundi
A, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge
zinatarajiwa kufikia tamati leo kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa.
Wenyeji na
mabingwa watetezi, Uganda The Cranes wanatarajiwa kumaliza na Sudan Kusini,
mchezo ambao utaanza saa 12:00 jioni, kabla ya hapo, kuanzia saa 10:00 jioni,
Kenya Harambee Stars wataonyeshana kazi na Ethiopia.
Uganda
wanaongoza Kundi A kwa pointi zao sita, wakifuatiwa na Ethiopia na Kenya, ambao
kila mmoja ana pointi tatu. Sudan Kusini hawana pointi hata moja.
Ikumbukwe
timu mbili za juu kutoka kila kundi, A, B na C zitafuzu moja kwa moja Robo
Fainali, wakati kutoka makundi yote matatu, watatafutwa washindi wa tatu bora
wawili, kukamilisha idadi ya timu za kucheza Nane Bora.
Kwa sababu
hiyo, pamoja na kwamba Sudan Kusini wamepoteza mechi zote mbili za mwanzo, bado
wanaweza kupigana kiume japo kugombea kupenya kama miongoni mwa washindi wa
tatu bora.
Kenya na
Ethiopia bila shaka patachimbika leo- kwani timu zote zimefungwa na Uganda na
zote zimeifunga Sudan Kusini- sasa leo itakuwa siku ya kujua nani nafuu kati
yao.
Mechi
nyingine za kukamilisha hatua ya makundi ya michuano hii, zitachezwa zote kesho
za Kundi B na C.
MSIMAMO
KUNDI A:
P W D L GF GA GD Pts
Uganda 2 2 0 0 2 0 2 6
Kenya 2 1 0 1 2 1 1 3
Ethiopia 2 1 0 1 1 1 0 3
Sudan Kusini 2 0 0 2 0 3 -3 0
MSIMAMO
KUNDI B:
P W D L GF GA GD Pts
Burundi 2 2 0 0 6 1 5 6
Tanzania 2 1 0 1 2 1 1 3
Sudan 2 1 0 1 1 2 -1 3
Somalia 2 0 0 2 1 6 -5 0
MSIMAMO
KUNDI C:
P W D L GF GA GD Pts
Zanzibar 2 1 1 0 2 1 1 4
Rwanda 2 1 0 1 3 2 1 3
Malawi 2 1 0 1 3 4 -1 3
Eritrea 2 0 1 1 2 3 -1 1
MECHI ZILIZOSALIA:
RATIBA
KUNDI B:
Desemba 1, 2012:
Sudan v Burundi (Saa 10:00
jioni)
Somalia v Tanzania (Saa
10:00 jioni)
RATIBA
KUNDI C:
Desemba 1, 2012:
Malawi v Zanzibar (Saa 10:00
jioni)
Eritrea v Rwanda (Saa
10:00 jioni)
VIWANGO VYA
UBORA FIFA
NCHI NAFASI
Uganda 86
Malawi 101
Ethiopia 102
Sudan 102
Rwanda 122
Burundi 128
Kenya 130
Tanzania 134
Zanzibar 134
Somalia 193
Eritrea 192
Sudan Kusini 200
(Viwango hivi vimetoka mwezi huu)