Uganda, mabingwa watetezi wanaanza na Kenya leo. Patachimbika Namboole |
Na Mahmoud
Zubeiry, Kampala
MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati,
Tusker Challenge inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo kwenye Uwanja wa Mandela,
uliopo Namboole, mjini Kampala, Uganda.
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Mcameroon, Issa
Hayatou tayari yupo mjini hapa kwa ajili ya kufungua michuano hiyo na jana
alihudhuria Mkutano Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA) katika hoteli ya Serena.
Wenyeji na mabingwa watetezi, Uganda ‘The Cranes’ watashuka
dimbani saa 12:00 jioni kupepetana na jirani zao, Kenya ‘Harambee Stars’ katika
mchezo mkali na wa kusisimua, kulingana na historia ya timu hizo zinapokutana.
Mchezo huo, utatanguliwa na mechi kati ya majirani wengine,
Sudan Kusini na Ethiopia itakayoanza saa Saa 9:00 Alasiri, ambayo nayo pia
inatarajiwa kuwa kali nay a kusisimua.
Mechi hizi za Kundi A, ambalo linastahili kuitwa Kundi la
kifo, zitafuatiwa na mechi za Kundi B kesho, kati ya Burundi na Somalia Saa
9:00 Alasiri na baadaye, saa 12 jioni Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’
watakuwa na kibarua kizito mbele ya Sudan.
Bara ambayo inajivunia kutwaa mara tatu Kombe la Challenge
katika miaka ya 1974, 1994 na 2010, iliwasili hapa jana jioni na kufikia katika
hoteli ya Mt Zion, ambako pia wamefikia Ethiopia, wawakilishi wa CECAFA katika
Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Januari mwakani nchini Afrika Kusini.
Stars iliyopangiwa kufanya mazoezi katika Uwanja wa Nakawa,
itarudi tena dimbani, Novemba 28 kukipiga na Burundi, mchezo utakaotanguliwa na
mechi kati ya Somalia na Sudan kabla ya kuhitimisha mechi zake za kundi hilo
kwa kumenyana na Somalia Desemba 1, mchezo utakaotanguliwa na mechi nyingine
kati ya Sudan na Burundi.
Michuano hii, imedhaminiwa na Kampuni ya Bia Afrika Mashariki
(EABL), kupitia bia yake ya Tusker Lager, kwa dau lao la dola za Kimarekani
450,000.
Udhamini wa mwaka huu huo ni ongezeko la aslimia 5, kutoka
michuano ya mwaka jana mjini Dar es Salaam, ambayo Uganda waliibuka mabingwa.
Ni udhamini ambao utahusu usafiri, malazi na huduma nyingine,
wakati jumla ya dola za Kimarekani 60.000 zitakuwa kwa ajili ya zawadi, bingwa
akipewa dola 30.000, mshindi wa pili dola 20.000 na dola 10.000 mshindi wa
tatu. Kama ilivyo ada, mechi zote za
michuano hiyo zitaonyeshwa na Televisheni ya Super Sport ya Afrika Kusini.
MAKUNDI
RATIBA TUSKER CHALLENGE 2012:
KUNDI A: Uganda,
Kenya, Ethiopia na Sudan Kusini
KUNDI B: Tanzania,
Sudan, Burundi na Somalia
KUNDI C: Malawi,
Eritrea, Rwanda na Zanzibar
RATIB KUNDI
A:
Novemba 24, 2012:
Ethiopia v Sudan (Saa
9:00 Alasiri)
Uganda v Kenya (Saa 12:00 jioni)
Novemba 27, 2012:
Sudan Kusini v Kenya (Saa
9:00 Alasiri)
Uganda v Ethiopia (Saa
12:00 jioni)
Novemba 30, 2012:
Kenya v Ethiopia (Saa
9:00 Alasiri)
Sudan Kusini v Uganda (Saa
12:00 jioni)
RATIBA
KUNDI B:
Novemba 25, 2012:
Burundi v Somalia (Saa
9:00 Alasiri)
Tanzania v Sudan (Saa
12:00 jioni)
Novemba 28, 2012:
Somalia v Sudan (Saa
9:00 Alasiri)
Tanzania v Burundi (Saa
12:00 jioni)
Desemba 1, 2012:
Sudan v Burundi (Saa 9:00 Alasiri)
Somalia v Tanzania (Saa
12:00 jioni)
RATIBA
KUNDI C:
Novemba 26, 2012:
Zanzibar v Eritrea (Saa
9:00 Alasiri)
Rwanda v Malawi (Saa
12:00 jioni)
Novemba 29, 2012:
Malawi v Eritrea (Saa
9:00 Alasiri)
Rwanda v Zanzibar (Saa
12:00 jioni)
Desemba 1, 2012:
Malawi v Zanzibar (Saa
9:00 Alasiri)
Eritrea v Rwanda (Saa
12:00 jioni)
ROBO
FAINALI:
Desemba 3, 2012
Mshindi Kundi C vs Mshindi wa Pili Kundi B (Saa
10:00 jioni)
Mshindi Kundi A vs Mshindi wa Tatu Bora wa pili (Saa
1:00 usiku)
Desemba 4, 2012 (16:00):
Mshindi Kundi B vs Mshindi wa Tatu Bora wa kwanza (Saa
10:00 jioni)
Mshindi wa Pili Kundi A vs Mshindi wa Pili Kundi C (Saa 1:00 usiku)
NUSU
FAINALI:
Desemba 6, 2012
Nusu Fainali ya Kwanza (Saa
10:00 jioni)
Nusu Fainali ya Pili (Saa
1:00 usiku)
MSHINDI WA
TATU:
Desemba 8, 2012
Waliofungwa Nusu Fanali (Saa 10:00 jioni)
FAINALI:
Desemba 8, 2012
Walioshinda Nusu Fainali
(Saa 1:00 usiku)
ORODHA YA MABINGWA
CHALLENGE;
Mwaka Bingwa
1973 Uganda
1974 Tanzania
1975 Kenya
1976 Uganda
1977 Uganda
1978 Malawi
1979 Malawi
1980 Sudan
1981 Kenya
1982 Kenya
1983 Kenya
1984 Zambia
1985 Zimbabwe
1986 Haikufanyika
1987 Ethiopia
1988 Malawi
1989 Uganda
1990 Uganda
1991 Zambia
1992 Uganda
1993 Haikufanyika
1994 Tanzania
1995 Zanzibar
1996 Uganda
1997 Haikufanyika
1998 Haikufanyika
1999 Rwanda B
2000 Uganda
2001 Ethiopia
2002 Kenya
2003 Uganda
2004 Ethiopia
2005 Ethiopia
2006 Zambia
2007 Sudan
2009 Uganda
2009 Uganda
2010 Tanzania Bara
2011 Uganda
2012 ?????
VIWANGO VYA
UBORA FIFA
NCHI NAFASI
Uganda 86
Malawi 101
Ethiopia 102
Sudan 102
Rwanda 122
Burundi 128
Kenya 130
Tanzania 134
Zanzibar 134
Somalia 193
Eritrea 192
Sudan Kusini 200
(Viwango hivi vimetoka mwezi huu)