Kavumbangu wa Yanga |
Na Mahmoud Zubeiry
CHIPUKIZI Seif Rashid wa Ruvu Shooting anakabana koo na
wachezaji wa kigeni wa klabu tatu bora nchini katika kuwania ufungaji bora wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam, Simba na Yanga.
Seif amefunga mabao matano na kati ya hayo, manne amefunga
dhidi ya tatu bora hao wa Ligi Kuu, Yanga mawili, Simba na Azam moja kila timu
na analingana na ‘mapro’ Kipre Tcheche wa Azam, Felix Sunzu wa Simba na Didier
Kavumbangu wa Yanga.
Wengine wenye mabao matano ni Amir Omary wa JKT Oljoro ya
Arusha na Amri Kiemba wa Simba SC,
wakati Hood Mayanja wa African Lyon FC ana mabao manne sawa na Peter Michael wa
Prisons FC, Emmanuel Okwi wa Simba SC na
Daniel Lyangawa Coastal Union.
Wengine wanaofukuzia tuzo hiyo, inayoshikiliwa na John
Raphael Bocco wa Azam ni Hussein Javu wa Mtibwa Sugar FC, Paul Ndauka wa Ruvu
Shooting, Paul Nonga wa JKT Oljoro FC,
Salum Kanoni wa Kagera Sugar, Nsa Job wa Coastal Union, Bocco mwenyewe ‘Adebayor’ na Mbuyu Twite wa Yanga,
ambao wote kila mmoja ana mabao matatu.
Wanaofuatia ni Jerry Santo wa Coastal Union, Abdulhalim Humud
wa Azam FC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Nizar
Khalfan wa Yanga, Hassan Dilunga wa Ruvu Shooting, Seleman Kibuta wa Toto
Africans, Mrisho Ngassa wa Simba SC, Themi Felix wa Kagera Sugar SC, Issa
Kanduru wa Mgambo Shooting, Jerry Tegete, Simon Msuva wa Yanga, Jamal Mnyate wa
Mtibwa Sugar na Said Swedi wa Coastal Union, ambao kila mmoja ana mabao mawili.
Waliofanikiwa kutikisa nyavu mara moja kila mmoja hadi sasa
ni Nassoro Masoud ‘Chollo’, Daniel Akuffo, Haruna Moshi ‘Boban’ wa Simba SC, Dickson Daudi wa Mtibwa Sugar,
Edward Christopher wa Simba SC, Freddy
Chudu wa Prisons, Nassoro Gumbo wa Mgambo Shooting FC, Said Ahmad, Omary Changa,
Credo Mwaipopo wa JKT Ruvu, Mohamed Netto, Robert Magadula wa Toto Africans, Amandus
Nesta wa Kagera Sugar, Kipre Bolou wa Azam FC, Elias Maguri wa Prisons, Mohamed
Hussein wa Toto Africans, Benedictor Mwamlangala wa Prisons na Ibrahim Hassan
wa JKT Oljoro.
Wengine ni Chande Magoja wa Mgambo Shooting, Shija Mkinna wa Kagera
Sugar, Haruna Adolf wa JKT Ruvu SC, Awadh
Juma wa Mtibwa Sugar, Meshack David wa JKT
Oljoro, Shaaban Nditi wa Mtibwa Sugar, Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting, Suleiman
Kassim ‘Selembe’ wa Coastal Union, Paul Nyangwe wa Polisi Morogoro, John Matei
wa Prisons, Hussein Swedi wa Ruvu Shooting, Salum Kipanga wa Mgambo Shooting, Severine
Constantine wa Toto Africans na Amos Mgisa wa JKT Ruvu FC.
Wengine ni Rafael Keyala wa Ruvu Shooting SC, Mussa Ngunda wa
Mgambo Shooting, Jimmy Shoji, Jacob Mambia wa JKT Ruvu, Fully Maganga wa Mgambo,
Juma Jabu wa Coastal Union, Salum Swedi wa Mtibwa Sugar FC, Lameck Dayton wa Coastal
Union, Ally Khan wa JKT Ruvu, Hamisi Kiiza wa Yanga, Wilfred Ammeh wa Kagera Sugar, Malimi Busungu wa Polisi
Morogoro, Said Suzan, Said Dilunga wa Ruvu Shooting, Mohamed Samatta wa African
Lyon FC, Malegesi Mwangwa wa Kagera Sugar, Said Bahanuzi wa Yanga, Mokili Rambo
wa Polisi Morogoro na Mohamed Mkopi wa Mtibwa Sugar.
Wachezaji ambao wamejifunga mabao hadi sasa katika Ligi Kuu
ni Cannavaro wa Yanga dhidi ya Toto mjini Mwanza, Jerry Santo wa Coastal dhidi
ya Azam Cghamazi na Hassan Ramadhan wa Mtibwa dhidi ya Toto African.
Felix Sunzu wa Simba kushoto akitibiwa na Dk Cossmass Kapinga katika moja ya mechi za timu hiyo |
WANAOWANIA KIATU CHA DHAHABU LIGI KUU:
MCHEZAJI MABAO TIMU
Amir Omary 5 JKT Oljoro FC
Kipre Tchetche 5 Azam FC
Seif Rashid u20 5 Ruvu Shooting SC
Didier Kavumbagu 5 Young
Africans SC
Felix Sunzu 5 Simba SC
Amri Kiemba 5 Simba SC
Hood Mayanja 4 African Lyon FC
Peter Michael 4 Tanzania Prisons FC
Emmanuel Okwi 4 Simba SC
Daniel Lyanga 4 Coastal union SC
Hussein Javu 3 Mtibwa Sugar FC
Paul Ndauka 3 Ruvu Shooting SC
Paul Nonga 3 JKT Oljoro FC
Salum Kanoni 3 Kagera Sugar SC
Nsa Job 3 Coastal
union SC
John Bocco 3 Azam FC
Mbuyu Twite 3 Young Africans SC
Kipre Tcheche wa Azam |