// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KILIMANJARO MARATHON KUFANYIKA MACHI 3 MWAKANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KILIMANJARO MARATHON KUFANYIKA MACHI 3 MWAKANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, November 16, 2012

    KILIMANJARO MARATHON KUFANYIKA MACHI 3 MWAKANI

    Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kushilla Thomas akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2013 katika ukumbi wa Serengeti, ndani ya hoteli ya JB Bellmonte, Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu wa Riadha Tanzania, Suleiman Nyambui na kushoto Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo, Juliana Yassoda na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe.  
    Na Mahmoud Zubeiry
    MASHINDANO ya Riadha ya 11 ya Kilimanjaro Marathon yanatarajiwa kufanyika Machi 3, mwakani mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
    Akizungumza kwenye uzinduzi wa mashindano hayo usiku huu katika hoteli ya JB Belmonte mjini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Kushilla Thomas alisema bia ya Kilimanjaro Premium Lager inaendelea na udhamini wa mbio hizo zinazoendelea kuwa kubwa na bora kila mwaka huku zikiibua vipaji vipya na kuwapa wanariadha chipukizi fursa ya kukua na kuweza kushindana kimataifa.
    “Kilimanjaro Premium Lager inalenga kuendeleza riadha kwa kukuza vipaji, kuwapa wanariadha wetu jukwaa la kushindania na wanariadha kutoka mataifa mbalimbali.” Alisema Kushilla.
    Aliongeza kuwa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ina lengo la kuhakikisha mashindano hayo yanakuwa na mvuto kwa wanariadha wenye vipaji ili kuongeza ubora wa riadha ya Tanzania ili Watanzania waweze kushiriki kikamilifu kwenye mashindano makubwa duniani.
    Kwa upande wake, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema: “Kupata washiriki kutoka nchi mbalimbali inatusaidia kuonyesha dunia kuwa Kilimanjaro Marathon nini lakini kuwaendeleza na kuwapa moyo wanariadha Watanzania ni kipaumbele chetu kikubwa, kwa sababu hiyo tumeanzisha zawadi maalum ya shilingi milioni 3 kwa Watanzania watakaomaliza wakiwa wa kwanza katika mbio za 42km Kilimanjaro Premium Lager Marathon na hii ni mbali na zawadi watayopata kwa nafasi watakazoshinda.”
    “Maandalizi ya Kilimanjaro Marathon 2013 yameishaanza ili kuhakikisha mbio hizo zinakuwa bora kama ilivyo utamaduni wetu kuhakikisha tunaboresha kila mwaka ili kuwapa raha ya aina yake washiriki pamoja na watazamaji.”
     “Kwa mara nyingine tena, Kilimanjaro Premium Lager itaendelea kuwathamini wanariadha kwa kuwatunuku zawadi nzuri ya fedha taslimu huku ikiwapa watazamaji burudani ya aina yake.”
    Zawadi ya fedha taslimu kwa washindi wa kwanza hadi wa tatu wanaume kwa wanawake kwenye mbio ndefu za km 42.195 zijulikanazo kama Kilimanjaro Premium Lager Marathon itakuwa ni shilingi milioni 3 , washindi wa pili watajipatia shilingi milioni 1.5 kila mmoja huku washindi wa tatu wakijipatia shilingi 850,000 kila mmoja. Zawadi nhii itakuwa ni kivutio kwa wanariadha mashuhuri kushiriki katika mbio hizi zinazoingia mwaka wa 11 tangu kuanzishwa.


    Utepe unakatwa

    Crew ya wadhamini wa Kili Marathon

    Kushilla akizungumza 

    Kavishe akizungumza

    Kushoto ni Rais wa PARALIMPIKI, Johonson Jasson na kulia na Nyambui

    Kavishe akizungumza na John Addison, Mkurugenzi wa Wild Frontiers, waandaaji wa Kili Marathon

    Mkurugenzi wa Executive Solutions, Aggrey Marealle akizungumza

    Mohamed Omar wa KK Security

    Walimbwende wa Executive Solutions

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KILIMANJARO MARATHON KUFANYIKA MACHI 3 MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top