Hamisi 'Diego' Kiiza |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
MSHAMBULIAJI
wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ amesema bao la nne aliloifungia timu yake, The
Cranes jana dhidi ya Sudan Kusini anawazawadia mashabiki wa klabu yake ambao
wanafuatilia mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA
Tusker Challenge, yanayoendelea mjini hapa.
“Mashindano
haya yanaonyeshwa na SuperSport dunia nzima, najua Watanzania wanafuatilia,
najua mashabiki wa klabu yangu wanafuatilia na kunisapoti, name kwa heshima
nataka nataka tushangilia pamoja lile bao,”alisema Kiiza.
Kiiza
alisema kwamba Yanga ni klabu ambayo inamlea vizuri na ndiyo maana ameendelea
kuwa mchezaji wa kiwango cha juu.
“Nawaheshimu
sana mashabiki wa Yanga, wamekuwa wakinihamasiaha kufanya vizuri kutokana na
jinsi wanavyonishangilia, na kufanya kwangu vizuri Yanga ndio kunaniweka The
Cranes siku zote,”alisema mchezaji huyo.
Kiiza jana
aliiongoza Uganda kufuzu kwa asilimia 100 hatua ya Robo Fainali ya Kombe la
CECAFA Tusker Challenge baada ya kushinda mechi zake zote za Kundi A, ikiwemo
ya jana waliyoshinda 4-0 dhidi ya Sudan Kusini.
Uganda na
Kenya wamefuzu moja kwa moja, wakati Ethiopia walioshika nafasi ya tatu
watasubiri hatima yao kufuzu kama mmoja wa washindi wa watatu bora kutoka
makundi yote, A, B na C.
Kiiza alifunga
bao lake dakika ya 79, wakati mabao mengine ya Uganda jana yalifungwa na Brian
Umony mawili katika dakika za 23 na 39 na Robert Ssentongo dakika ya 47.
Katika mechi
ya kwanza, Kenya ilishinda 3-1 dhidi ya Ethiopia, mabao ya Ramadhan Mohamed
Salim, Clifton Miheso na David Ochieng, wakati la Ethiopia lilifungwa na Gatech
Panom Yietch.
Michuano
hiyo, itaendelea leo kwa mechi za Kundi B na C, saa 8:00 mchana, Tanzania Bara
watamenyana na Somalia Uwanja wa Lugogo na baadaye saa 10:00, Rwanda itacheza
na Eritrea wakati Sudan itaanza na Burundi saa 8:00 mchana Uwanja wa
Wankulunkulu na baadaye saa 10:00 jioni Malawi watamenyana na Zanzibar
Wankulunkulu.