Kikosi cha Kenya |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
KENYA wako
hatarini kupokonywa uenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati,
CECAFA Tusker Challenge mwakani na badala yake wakapewa Rwanda.
Habari
kutoka kwenye Mkutano wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA) uliofanyika Ijumaa iliyopita, zimesema kwamba Rwanda wameambiwa wakae
tayari kwa uenyeji wa michuano hiyo, iwapo Kenya itachemsha.
Habari zinasema
Mwenyekiti wa Shirikiasho la Soka Kenya (FKF), Sam Nyamweya, awali alisema
katika Mkutano Mkuu wa CECAFA kwenye hoteli ya Serena, kwamba Kenya tayari
imekwishapata mfadhili wa mashindano hayo.
Kasha
baadaye, Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Rwanda, FERWAFA, Celestin Ntagungira,
akasema itakuwa tayari kutaja jina la mdhmaini
wa Challenge ndani ya wiki mbili wakipewa uenyeji.
Katika
kuamua utata huo, Rais wa CECAFA Injinia Leodegar Tenga alisema haki za uenyeji
wa Challenge ya mwakani zitakwenda kwa nchi ambayo kwanza itawahakikishia
mdhamini wa mashindano.