KLABU ya Yanga leo imemtangaza Shaaban Katwila kuwa Meneja wa Timu A na Baraka Kizuguto kuwa Afisa Mawasiliano wa klabu, kujaza nafasi zilizkokuwa wazi kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja.
Akiongea na waandishi wa habari, Kaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Lawrence Mwalusako, amesema kikao cha Kamati ya Utendaji kilichoketi mwishoni mwa wiki kiliwapendekeza Katwila na Kizuguto kushika nafasi hizo zilizokua wazi.
Katwila anakuwa Meneja wa timu kufuatia kuwa wazi kwa nafasi hiyo baada ya aliyekuwa meneja wa timu Hafidh Saleh kuhamishiwa idara ya Mipango na Usafirishaji na Kizuguto anachukua nafasi iliyokua wazi kufuatia Louis Sendeu kumalizika kwa mkataba wake.
Aidha Mwalusako alisema Katwila ana uzoefu na masuala ya mpira, alikuwa mchezaji wa Yanga kwa kipindi kirefu, alikuwa Nahodha wa timu ya Yanga na timu ya mkoa wa Dar es Salaam kwa vipindi tofauti hivyo anauelewa na masuala ya mpira na atakua kiunganishi kizuri kati ya Uongozi na wachezaji.
Kizuguto ana taaluma ya Teknlojia, Habari na Mawasiliano hibyo Kamati ya Utendaji iliona anafaa kushika nafasi ya Habari na Mawasilliano, kwa kuwa ana uzoefu na masuala ya mawasiliano ya jamii kufuatia kazi hiyo kwa muda mrefu alisema 'Mwalusako'
Naye Katwila alishukuru kwa uongozi kumwamini na kumpa nafasi hiyo, na kusema anaamini ataifanya vizuri ipasavyo kwa kuwa ana uzoefu na masuala ya michezo na uongozi.
Afisa Mawasiliano mpya wa Yanga Kizuguto ameishukuru Kamati ya Utendaji kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo ambapo amomba ushirikiano kwa vyombo ya habari, uongozi na wanachama katika kufanikisha malengo ya kuifanya klabu ya Yanga kwenda mbele zaidi