Benny Kisaka |
Na Mahmoud Zubeiry
MWENYEKITI wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo
Tanzania (TASWA), Juma Abbas Pinto amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwakilishi
wa Klabu katika uchgauzi wa Chama cha Soka Dar es Salaam.
Juma Pinto |
Winga huyo wa timu ya mkoa wa Dar es Salaam, Mzizima United
iliyoshiriki Kombe la Taifa, Taifa Cup mwaka 1997 mkoani Kagera, kwa kuchukua fomu
ya kuomba nafasi hiyo, ina maana atachuana na Mkurugenzi wa kampuni ya Jambo
Concepts Limited, Benny Kisaka, ambaye pia ni Mwana Habari.
Wagombea wengine katika nafasi hiyo ni Philemon Ntahilaja na
Frank Mchaki, wakati wanaowania Ujumbe wa Mkutano Mkuu ni Isaac Mazule, Shufaa
Jumanne, Shaffi Dauda na Muhisn Balhabou, huku Shaaban Mohamed, Andrew Tupa,
Siza Abdallah Chenje, Sunday Mwanahewa, George Wakuganda na Lameck Nyambaya wakiwania
Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
Wanaowania Uenyekiti ni Ahmad Seif Hemed ambaye anachuana na Brown
Ernest, Salum Mkemi, Evans Aveva, Ayoub Nyenzi, Juma Jabir na Meba Ramadhan, wakati
nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Ally Mayay na Salum Mwaking’inda, na Ukatibu
Mkuu, Said Tuliy na Hamisi Ambari ndio waliojiotokeza hadi sasa, ingawa kuna
habari Rahim Kangezi ‘Zamunda’ naye atachukau fomu.
Uchaguzi wa DRFA utafanyika Desemba 8, mwaka huu na fomu za
kugombea nafasi mbalimbali zilianza kutolewa tangu Oktoba 29, wakati Novemba 4
hadi 8, Kamati ya Uchaguzi, chini ya Mwenyekiti wake, Juma Simba itapitia fomu
za walioomba uongozi.
Novemba 9 hadi 13 utakuwa muda wa pingamizi kwa wagombea,
ambazo zitajadiliwa Novemba 14 hadi 16, wakati Novemba 17 hadi 19 watatoa fursa
ya kukata rufaa, ambazo zitasikilziwa Novemba 20 hadi 24 na baada ya hapo,
Novemba 25 yatatangazwa majina ya wagombea waliopitishwa.
Uchaguzi wa DRFA utafanyika siku chache tu kabla ya uchaguzi
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mwishoni mwa Desemba, mwaka huu.