// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); JICHO LA MDAU WA BIN ZUBEIRY KATIKA LIGI KUU MZUNGUKO WA KWANZA NA MAONI YAKE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE JICHO LA MDAU WA BIN ZUBEIRY KATIKA LIGI KUU MZUNGUKO WA KWANZA NA MAONI YAKE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, November 12, 2012

    JICHO LA MDAU WA BIN ZUBEIRY KATIKA LIGI KUU MZUNGUKO WA KWANZA NA MAONI YAKE

    Na Ricardo Makivic
    Mimi Mpenda maendeleo wa soka la Tanzania, na mwana harakati kunyenyua Soka letu, nina machache ya kuongea baada ya Raundi hii ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzanzia Bara.

    1. Yangu kwa Coastal union;
    Kwa Kweli kama mulivyo ahidi msimu huu CUFC itakuwa zaidi ya msimu ulio pita, kweli maendeleo tumeyaona, hata kama msimu huu hauja isha....Kwa kweli, mimi binafsi napenda timu zenye malengo fulani afu zinajituma kwa namna moja au nyingine kutimiza Malengo hayo.
    Atupele Green, mshambuliaji wa Coastal Union
     
    Coastal Union imeonyesha nia na pia, imejaribu kutekeleza kwa jinsi ya uwezo wao, kwa kweli wenye tumeona "Ukiwa na Nia, na Pia ukajituma basi yoyote yanawezekan", Uwezo wa Coastal Union kuchukua ubingwa msimu huu, upo - naweza nikaonekana mjinga lakini kuna maana. Ni kwamba, itahitaji timu ijipange vizuri, iwe na vitu kwa maneno ya kiingereza 'Consistency' na pia 'Resilience', huu ni uwezo wa timu kuendeleza kucheza mpira mzuri na kupata matokeo mazuri, pia uwezo wa timu kujipanga upya pale wanapo poteza mchezo.
    Hivi ndo vitu muhimu ambavyo timu zenye mafanikio zinaweza kutekeleza.
    Hongera kwa hilo, Ligi haijaisha (ndio mwanzo), endeleeni bila kukata tamaa - malengo yenu mutafikia.


    2. Yangu kwa Azam;
    Kwa kweli, Azam ni timu ambayo niliiwekea nafasi ya kwanza kabisa ichukue ubingwa msimu huu, kwa rekodi nzuri tuu, ila niseme Azam wananiangusha - pia washabiki wote wa soka Tanzania wanaopenda maendeleo.
    Kwa kweli sijaona kitu ambacho kinaweza kuwa nyima Azam msimamo na kushindwa kupindua mpira wa Tanzania. Hata Abedi Pele mwenyewe kasema hilo.
    Mshambuliaji wa Azam, John Bocco

    Kwa kweli, kitu kinacho wasumbua Azam kwa Sasa ni 'Utulivu na Msimamo' (Stability in the team)...Azam inahitaji iwe na utulivu kuanzia katika Uongozi, mpaka wachezaji, na wote wajitume (Hardwork), umoja (Teamwork), na pia kuwa na nia/roho ya Ushindi (spirit of success) hata mazingira yabadilike vipi, bado msimamo uwepo.
    Hata klabu maarufu na kubwa duniani mfano mzuri ni Inter na AC Milan ambazo kwa miaka miwili iliyo pita ili kosa msimamo kuanzia uongozi na wachezaji pian na tumeona jinsi zinavyo angaika, Inter ilichukua UEFA lakini sana ipo Europa League, Milan wao wanahangaika kupanda juu.
    Kwa kweli Azam musipo angalia, itakuwa hivyo, kinacho faa sasa ni kukaa kama Uongozi pia na wachezaji, futeni tofauti na rekebisheni makosa, pia kuwaasa wachezaji wawe na moyo wa mafanikio, kujituma pia kuwa na nidhamu. Kuwaambia kuwa “kama nikutaka mafanikinio, tunayatengeza wenyewe kwa pamoja - kama hatu yataki, tunaya fukuza wenyewe” (Umoja ni muhimu).
    Kwa kweli, Azam inahitaji kutulia na raundi ya pili tuone mabadiliko, kuna msemo huu na nukuu: "Success is the sum of small efforts, repeated day in and day out." - Robert Collier.
    AZAM INA WEZA! Nafasi hiyo yapili, itunze pia itafuteni hiyo nafasi ya kwanza kwa nguvu na moyo. Mutaipata.


    3. Yangu Kwa Simba na Yanga
    Hizi ndo timu mama za mpira wa Tanzania, na pia ndo timu zinazofahamika sana Duniani kwenye swala zima la mpira wa Tanzania.
    Kikosi cha Simba SC
    Tuache maneno, tunza nidhamu, tunzeni heshima zenu, pia za nchi yenu. Sio vizuri timu kubwa kuwa mfano mbaya, au kuhusika katika mambo yanashusha hadhi zenu.
    Rekebisheni hayo, Chezeni mpira mzuri, kwa kufuata kanuni za Soka (FIFA pia TFF), na mutaonekana kama nyota Afrika na Duniani....mfano: TP Mazembe ya Congo inafahamika vizuri Duniani na imekuwa na mafanikio, hii ni kwajili ya kufuata hayo mambo. Simba - Yanga n.k zaweza.
    Endelezeni juhudi, jiandaeni Raundi ya pili pia na Mashindano ya Afrika (CAF Champs Lge) kwa simba. Wengine kujipanga ili kupata nafasi hiyo ya kuwakirisha nchi Afrika.

    4. Maoni kwa mashabiki/wapenzi/Wadau wa Soka nchini Tanzania.
    mashabiki hujenga timu, na pia hubomoa. Pia huchangia katika kubadirisha matokeo katika mechi, mfano katika mechi yetu iliyopita ya Kitaifa Taifa Stars dhidi ya Gambia, washabili walichangia kupandisha morali ya wachezaji na kuwatia moyo na nguvu pia kupata ushindi, hii imetuweka katika nafasi nzuri katika kukombania ticketi Kombe la Dunia 2014 Brazil....kwa mara ya pili, nawezekana niaonekana kama mjinga lakini kuna ukweli: Hakuna lisilowezekana, kwa nini waweze wao sisi tushindwe?? Swali la kujiuliza.
    Mashabiki wa Yanga Uwanja wa Taifa nyuma ya tim

    Mashabiki tuchukue nafasi zetu, tutoe 'Ushabiki wa Kijinga' kuni radhi, kufute tofauti zetu pale timu ya taifa inapo cheza bila kujali mchezaji gani kapangwa ana cheza au la au ametokea timu gani, na uhakika kuwa Kocha Kim Poulsen anafanya kazi yake vizuri mno.

    Tumbuke, timu yetu ya Taifa ikiingia kwenye World Cup wote tutakuwa tunaangalia, na kushangilia hata kama mechi zitakuwa zinaonyesha alfajiri kwa muda wetu wa Afrika mashariki.

    TANZANIA INAWEZA!!!!
    Hii sio kwa timu ya taifa tu bali hata kwa vilabu. Tusiwe wajinga kwa sababu ya Ushabiki eti akija mgeni ndo una mpenda sana kuliko mzaliwa nae! Mfano kwa mashindano, kama timu yako imetolewa au imeshindwa kushiriki basi, pale timu ya nyumbani inapocheza ipewe mkono, sio kuzomea wa nyumbani, na kushangilia wageni. Tukifanya hivi tutanyenyua Soka Tanzania.

    5. Mwisho.
    Mpira wa Miguu Tanzania upo katika mbio za kusaka maendeleo, hata Abedi Pele alisema, kuwa Ghana, Misri na nchi zote kubwa kisoka Afrika zilianza hivi, lakini pia Shirikisho la soka Tanzania (TFF) liendeleze juhudi zake, na uongozi ufanye kazi kwa Uadilifu pia viongozi wote wa soka nchin hadi kwenye vilabu.
    Ningependa kuchukua mfano kwa maneno aliyo tamka Rais wa Marekani Barak Obama aliporudi ikulu na kumfanya atoe machozi, alisema kuwa alitaka Wafanyakazi wote na viongozi wote - wafanye kazi kwa uadilifu, kujituma, uaminifu, na kwa umoja wakati anaporudi madarakani kwa mara ya pili.
    Hapa, kwa Lugha nyingine 'Katika Safari ya kuleta maendeleo katika sekta fulani, inahitaji viongozi kufanya kazi zao vizuri zaidi.'
    Shirikisho La Soka Tanzania (TFF) liongeze bidii na kuendeleza programu mbalimbali za kuinua soka nchini.
    Ni hayo tu maoni yangu, Shukrani kwa wote walio soma makala hii.
    MUNGU IBARIKI SOKA LA TANZANIA, Amina.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: JICHO LA MDAU WA BIN ZUBEIRY KATIKA LIGI KUU MZUNGUKO WA KWANZA NA MAONI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top