Ally Kimera asiyefungika |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
KIPA namba
mbili wa Uganda, Ally Kimera ameendelea kushika vizuri mikoba ya kipa namba
moja nchi hiyo, Abbel Dhaira kwa kuwa mlinda mlango pekee ambaye hajafungwa
hadi sasa katika mashindano haya.
Kimera
alimpokea Dhaira kipindi cha pili katika mchezo wa kwanza wa Kundi A dhidi ya
Kenya na ameendelea kudaka mechi mbili zaidi hadi kumaliza hatua ya makundi,
akiwa hajaruhusu nyavu zake kuguswa hata mara moja.
Huyu sasa
anajitengenezea mazingira mazuri ya kuwa kipa bora wa mashindano haya,
yaliyoanza Novemba 24 na yanatarajiwa kutia nanga Desemba 8, mwaka huu mjini
hapa.
Kipa wa
Kenya, Duncan Ochieng ametunguliwa mabao mawili katika mechi tatu alizodaka,
kipa wa Ethiopia, Samson Asefa Worku, ametunguliwa mabao matatu katika mechi
tatu na kipa wa Sudan Kusini, Juma Ginaro anashika rekodi ya kufungwa mabao
mengi, saba na timu yake imetolewa.
Kipa wa
Burundi, Arthur Arakaza amefungwa bao moja katika mechi mbili, kipa wa
Tanzania, Juma Kaseja amefungwa bao moja pia, tena kwa penalti, katika mechi
mbili, kipa wa Sudan, Abd Elrahman Ali amefungwa mabao mawili katika mechi
mbili, wakati kipa wa Somali, Moalim Abdullahi amefungwa mabao sita.
Kipa wa
Zanzibar Mwadini Ally amefungwa bao moja, kipa wa Rwanda, Jean Claude Ndoli
amefungwa mabao mawili, kipa wa Malawi, Charles Swini amefungwa mabao manne na
kipa wa Eritrea, Fitsum Kelati amefungwa mabao matatu.
Lakini
makipa wa timu za Kundi B na C wana jukumu la kulinda milango yao katika mechi
za mwisho za makundi yao, ili kuzilinda rekodi zao pia.