Mwigizaji wa filamu hiyo, Henry Babuu kushoto na Barbra
Kalugira kulia, Meneja Masoko na Mratibu wa filamu hiyo
|
Isakwisa Kanyenyela kushoto na Adam Semkwiji ‘Snare’ na
Innocent Nyika, waliohusika katika idara za kitaalamu kwenye kutayarisha filamu
hiyo.
|
Na Princess Asia
KAMPUNI ya Afronode Films, imeandaa filamu maalum
iliyopachikwa jina la Shujaa ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Jakaya Kitwete kwa kuhamasisha wananchi kupima ukimwi kwa hiyari.
Akizungumza mjini Dar es salaam leo, Meneja Masoko wa kampuni
hiyo, Barbra Kalugira, alisema kuwa kila kitu kimekamlika ambapo uzinduzi wake
utafanyika Desemba mosi ambayo ni siku ukimwi duniani.
Kalugira alisema kuwa katika filamu hiyo itazungumzia watu
kwenda kupima kwa hiyari kama alivyofanya Rais wa Tanzania ambaye ndiye
kiongozi pekee katika ukanda wa Afrika kuhamasisha kupima ukimwi.
"Ni kitendo cha kumpongeza sana Rais wetu kwa kwenda
kupima kwa hiyari na kuhamasisha wananchi wote wajitokeze kupima hivyo tunazindua
filamu hiyo ambayo inazungumzia janga la ukimwi na madhara ya
kutopima"alisema Kalugira.
Pia Kalugira alisema kuwa katika filamu hiyo itamzungumzia
kijana mmoja ambaye alikataa kwenda kupima alipokutana na msichama ambaye ni
muadhirika wa ukimwi.
Alisema mpaka kukamilika kwa filamu hiyo jumla ya sh.milioni
35 zimetumika katika kukamilisha.
Kalugira alisema kuwa mpaka wiki ijayo watakuwa wamejua ni
wapi watafanya uzinduzi huo.
"Filamu yetu inaitwa Shujaa ambayo tutazindua Desemba Mosi
(2012), lakini bado hatujajua ni wapi tutafanyia uzinduzi huo ambao unaujumbe
mkubwa kwa jamii kuhusiana na janga zima la Ukimwi"alisema Kalugira.