KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema atastaajabu sana iwapo Robin van Persie hatapata mapokezi mazuri mbele ya mashabiki wa Arsenal kesho.
SOURCE: http://www.dailymail.co.uk
Mholanzi huyo mkali wa mabao anavaana na klabu yake ya zamani kwa mara ya kwanza, tangu ahamie United kwa dau la uhamisho la pauni Milioni 24 msimu huu, Gunners ikizuru Old Trafford katika Ligi Kuu ya England Jumamosi.
Van Persie amewafungia mabao 37 wababe hao wa London msimu uliopita, na mkataba wake ukiwa unaelekea ukingoni, alikataa kuongeza na kuuzwa kwa mahaismu.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 tangu hapo amekuwa na mwanzo mzuri United, akifunga mabao tisa katika mechi 12.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema Van Persie, ambaye alitua England akitokea Feyenoord baada ya kununuliwa na The Gunners mwaka 2004 anastahili heshima na Ferguson amekubali hilo.
Van Persie |