Kaseja |
Na Mahmoud Zubeiry
KIPA wa
zamani wa Simba na aliyekuwa kocha wa makipa wa timu hiyo, Iddi Pazi ‘Father’
amesema kwamba uwezo wa kipa namba moja wa sasa klabu hiyo umeshuka na tiba
yake anaijua.
“Kaseja
uwezo umeshuka kidogo, kwa sababu daktari wake sipo pale, Simba wakinirudisha
kazini, Kaseja atafufua makali yake na atakuwa hafungiki kwa urahisi,”alisema
Pazi.
Pazi
ameushauri uongozi wa Simba umerejeshe kazini ili aokoe kipaji cha kipa huyo
bora, miongoni mwa walinda milango bora kuwahi kutokea Tanzania.
Kwa sasa,
kocha wa makipa wa Simba ni kipa mwingine wa zamani wa Simba, James Kisaka
ambaye alipewa kazi hiyo baada ya Pazi kwenda Oman. Lakini kwa sasa Pazi
amemaliza mkataba wake Oman na yupo nyumbani kwake, Majumba Sita, Ukonga, Dar
es Salaam.
Katika mechi
12, Kaseja amefungwa mabao 10 kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzanoia Bara msimu
huu, kitu ambacho si kawaida yake katika misimu iliyotangulia, ingawa hiyo
inaelezwa inachangiwa hata na ubutu wa safu ya ulinzi ya sasa wa timu
hiyo.
Lakini pia, kocha
Mserbia wa Simba SC, Profesa Milovan Cirkovick naye anadaiwa kuchangia matokeo
mabaya na habari zinasema anaweza kutimuliwa wakati wowote kwenye klabu hiyo,
kufuatia kutofautiana na uongozi wa klabu hiyo.
Uongozi wa
Simba unamtuhumu Mserbia huyo kwamba ni mbishi hashauriki na hilo limekuwa
likiigharimu timu katika michezo yake ya karibuni ya Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara.
“Huyu jamaa
tumemvumilia sana, mimi sina hamu naye tena, sijui wenzangu. Anapanga kikosi
ovyo na ndiyo chanzo cha matokeo haya mabaya,”alisema kiongozi mmoja wa
Simba.
Lakini kwa
upande mwingine, inadaiwa matokeo haya mabaya ya Simba ni matokeo ya mgomo wa
wachezaji wakishinikiza wachezaji wenzao waliosimamishwa Haruna Moshi ‘Boban’
na Juma Nyosso warejeshwe kikosini.
Zaidi Boban,
wachezaji wanadaiwa kumpenda sana kutokana na roho yake safi ya kibinadamu na
upendo mkubwa kwa wenzake.
Boban ndiye
mchezaji pekee aliyejitolea kuusindikiza nyumbani kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo (DRC) mwili wa marehemu Patrick Muteesa Mafisango, kiungo wa Simba
aliyefariki dunia Mei mwaka huu kwa ajali ya gari.
Simba SC juzi
ilifungwa mechi ya kwanza ya Ligi Kuu mabao 2-0 na Mtibwa Sugar, Uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro, mabao ya Said
Mkopo na Hussein Javu.
Simba
inabaki na pointi zake 23, baada ya kucheza mechi 12, ikiipisha kileleni Yanga
yenye pointi 26 sasa. Simba itamaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kwa kumenyana
na Toto African Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.