// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); DOGO ASLAY AULA KORA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE DOGO ASLAY AULA KORA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, November 02, 2012

    DOGO ASLAY AULA KORA

    Dogo Aslay

    Na Princess Asia
    MSANII chipukizi wa Bongo Fleva, Dogo Aslay kutoka kundi la Wanaume Family TMK, ameteuliwa kuwania tuzo za muziki Afrika (KORA) kupitia kipengele cha Msanii Bora Anayechipukia kutoka Afrika Mashariki.
    Dogo huyo anayewakuna kuanzia watoto hadi wakubwa kwa nyimbo zake ‘tamu’, ameingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za KORA ambazo hutolewa Afrika Kusini, kupitia wimbo wake wa Niwe NaweI ambao ‘unabamba’ ile mbaya.
    Meneja wea Kundi la Wanaume Family, Said Fela ameiambia BIN ZUBEIRY mida hii kwamba Aslay amepokea kwa furaha kubwa matokeo hayo na anawashukuru Watanzania kwa kuikubali kazi yake.
    Fela amesema Asaly anawashukuru pia waandaaji wa tuzo hizo kwa kuithamini kazi yake na kuiingiza katika orodha ya kazi bora Afrika, kwani hiyo ni heshima kubwa kwake na kwa taifa lake.  
    Pamoja na hilo, Aslay ameomba Watanzania wafuatilie mchakato wa tuzo hizo ili kujua namna ya kumpigia kura, hatimaye anyakue tuzo hiyo.
    “Naomba wapenzi wa muziki nchini kwa ujumla wafuatilie mchakato huo ili waweze kumpa sapoti Dogo abebe tuzo hiyo na kuzidi kuitangaza Tanzania katika medani ya kimataifa ya muziki,”alisema Fela. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: DOGO ASLAY AULA KORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top