// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CHUJI AWAWEKEA NADHIRI AZAM - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CHUJI AWAWEKEA NADHIRI AZAM - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, November 02, 2012

    CHUJI AWAWEKEA NADHIRI AZAM

    Chuji kulia akimburuza kiungo wa JKT Mgambo juzi

    Na Mahmoud Zubeiry
    KIUNGO wa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’, amesema kwamba mechi yao ya Jumapili dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itakuwa ngumu, lakini watapigana kwa nguvu zao zote washinde ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana kutoka kambini kwao, Bagamoyo mkoani Pwani, Chuji alisema kwamba Azam ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri, hususan katika nafasi ya kiungo, hivyo wanatarajia upinzani mkali siku hiyo.
    “Azam wazuri, wana viungo vizuri na mbaya zaidi wanapokuwa wanacheza na sisi wanakomaa zaidi, wazi mchezo utakuwa mgumu,”alisema mtoto huyo wa winga wa zamani wa CDA ya Dodoma, Iddi Athumani na kaka wa mshambuliaji wa Coastal, Pius Kisambale.
    Amesema anatarajia upinzani mkali kutoka viungo wa Azam kama Salum Abubakar ‘Sure Boy’, lakini watakabiliana nao na watawaonyesha kwamba Yanga ni zaidi.
    “Tumepigana sana hadi kufika hapa, tulianza ligi vibaya, sasa hivi tunataka kuiacha mbali kabisa Simba, kwa hivyo tumedhamiria sana kuwafunga Azam Jumapili,”alisema Chuji.
    Akiizungumzia Ligi Kuu kwa ujumla, Chuji alisema ni ngumu na wanashukuru wao walianzia mechi ngumu zaidi za mikoani ambako walipokuwa wanapata matokeo mabaya wengi waliwadharau na kuwakebehi.
    “Sisi tumetoa droo na Prisons, tumefungwa na Mtibwa na Kagera tukachekwa sana, sasa na wenzetu (Simba) wameenda mikoa miwili tu, lakini sasa tunalingana pointi, kiko wapi sasa walichokuwa wanatucheka, hao hawajaenda Kanda ya Ziwa, hawajaenda Arusha, hawajaenda Mbeya, unategemea nini?”alisema Chuji.
    Pamoja na hayo, Chuji amesema wanaamini mechi zote za Ligi Kuu ni ngumu na wamejipanga kucheza kwa nguvu ile ile kila mechi, ili kuhakikisha wanashinda zote zilizobaki.
    Yanga itamenyana na Azam Jumapili Uwanja wa Taifa, mechi ambayo inatarajiwa kuwa kali na ya kusisimua, kutokana na upinzani wa karibuni baina ya timu hizo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: CHUJI AWAWEKEA NADHIRI AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top