Uganda, mabingwa wa kihistoria wa Challenge |
NA
MAHMOUD ZUBEIRY
MICHUANO
ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama CECAFA
Challenge Cup, mwaka huu itafanyika mjini Kampala, Uganda kuanzia Novemba 24
hadi Desemba 8.
Kampuni
ya Bia Afrika Mashariki (EABL), kupitia bia yake ya Tusker Lager, ndio
wadhamini michuano hiyo kwa dau lao la dola za Kimarekani 450,000 walizitoa kwa
ajili ya michuano ya mwaka huu ya Kombe la CECAFA –Tusker Challenge Cup.
Katibu
wa CECAFA, Nicholas Musonye alisema mapema tu wakati wa maandalizi ya awali ya
michuano hiyo, kwamba lengo la michuano hiyo ni kuzisaidia maandalizi timu za
Afrika Mashariki na Kati katika kuwania tiekti ya kucheza Fainali za Kombe la
Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Udhamini
wa mwaka huu huo ni ongezeko la aslimia 5, kutoka michuano ya mwaka jana mjini
Dar es Salaam, ambayo Uganda waliibuka mabingwa.
Ni
udhamini ambao utahusu usafiri, malazi na huduma nyingine, wakati jumla ya dola
za Kimarekani 60.000 zitakuwa kwa ajili ya zawadi, bingwa akipewa dola 30.000,
mshindi wa pili dola 20.000 na dola 10.000 mshindi wa tatu. Kama ilivyo ada, mechi zote za michuano hiyo
zitaonyeshwa na Televisheni ya Super Sport ya Afrika Kusini.
Michuano
hiyo huandaliwa na CECAFA, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati,
ambalo lina wanachama 12.
Japokuwa
ukanda wa CECAFA ndiyo eneo linalojikongoja kwa sasa katika soka ya kimataifa,
lakini ukweli ni kwamba, mpira wa miguu barani Afrika, ulianzia ukanda wa
Afrika Mashariki.
Michuano
ya kwanza kabisa mikubwa barani Afrika, ilihusisha mataifa manne, Kenya , Uganda ,
Tanganyika (sasa Tanzania
Bara) na Zanzibar ,
ikijulikana kwa jina la Kombe la Gossage.
Michuano
hiyo ya Gossage ambayo sasa imekuwa Kombe la Challenge, ilifanyika mara 37
kuanzia mwaka 1926 hadi 1966, ilipobadilishwa jana na kuwa michuano ya wakubwa
ya soka kwa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, ilifanyika mara saba kati ya
mwaka 1965 na 1971, ilipozaliwa rasmi CECAFA Challenge.
Michuano
hiyo ilikuwa ikidhaminiwa na bepari aliyekuwa akimiliki kiwanda cha sabuni,
William Gossage, aliyezaliwa Mei 12 mwaka 1799 na kufariki dunia Aprili 9,
mwaka 1877.
Michuano
hiyo mikongwe zaidi barani, imekuwa ikiandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka
Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), ikihusisha timu za taifa za ukanda huo.
Hadi
inafikia tamati michuano ya Gossage , Uganda ilikuwa inaongoza kwa kutwaa taji hilo , mara 22, ikifuatiwa na Kenya
iliyotwaa mara 12 na Tanzania
mara tano.
Mwaka
2005, michuano hiyo ilifanyika chini ya udhamini wa bilionea wa Ethiopia mwenye
asili ya Saudi Arabia, Sheikh Mohammed Al Amoudi na kupewa jina la Al Amoudi
Senior Challenge Cup, lakini sasa Tusker ndiyo mambo yote.
MABINGWA
CHALLENGE;
Mwaka
Bingwa
1973
Uganda
1974
Tanzania
1975
Kenya
1976 Uganda
1977
Uganda
1978
Malawi
1979
Malawi
1980
Sudan
1981
Kenya
1982
Kenya
1983
Kenya
1984
Zambia
1985
Zimbabwe
1986 Haikufanyika
1987
Ethiopia
1988
Malawi
1989
Uganda
1990
Uganda
1991
Zambia
1992
Uganda
1993 Haikufanyika
1994
Tanzania
1995
Zanzibar
1996
Uganda
1997 Haikufanyika
1998 Haikufanyika
1999
Rwanda B
2000
Uganda
2001
Ethiopia
2002
Kenya
2003
Uganda
2004
Ethiopia
2005
Ethiopia
2006
Zambia
2007
Sudan
2009
Uganda
2009
Uganda
2010 Tanzania Bara
2011 Uganda
KUNDI A: Uganda, Kenya, Ethiopia na
Sudan Kusini
KUNDI B: Tanzania, Sudan, Burundi na
Somalia
KUNDI C: Malawi, Eritrea, Rwanda na
Zanzibar
RATIB KUNDI A:
Novemba 24,
2012:
Ethiopia
v Sudan (Saa 9:00 Alasiri)
Uganda
v Kenya (Saa
12:00 jioni)
Novemba 27,
2012:
Sudan
Kusini v Kenya (Saa 9:00 Alasiri)
Uganda
v Ethiopia (Saa
12:00 jioni)
Novemba 30,
2012:
Kenya
v Ethiopia (Saa
9:00 Alasiri)
Sudan
Kusini v Uganda (Saa 12:00 jioni)
RATIBA KUNDI B:
Novemba 25,
2012:
Burundi
v Somalia (Saa 9:00 Alasiri)
Tanzania
v Sudan (Saa 12:00 jioni)
Novemba 28,
2012:
Somalia
v Sudan (Saa
9:00 Alasiri)
Tanzania
v Burundi (Saa 12:00 jioni)
Desemba 1,
2012:
Sudan
v Burundi (Saa
9:00 Alasiri)
Somalia
v Tanzania (Saa 12:00 jioni)
RATIBA KUNDI C:
Novemba 26,
2012:
Zanzibar
v Eritrea (Saa 9:00 Alasiri)
Rwanda
v Malawi (Saa 12:00 jioni)
Novemba 29,
2012:
Malawi
v Eritrea (Saa
9:00 Alasiri)
Rwanda
v Zanzibar (Saa 12:00 jioni)
Desemba 1,
2012:
Malawi
v Zanzibar (Saa 9:00 Alasiri)
Eritrea
v Rwanda (Saa 12:00 jioni)
ROBO FAINALI:
Desemba 3,
2012
Mshindi
Kundi C vs Mshindi wa Pili Kundi B (Saa 10:00 jioni)
Mshindi
Kundi A vs Mshindi wa Tatu Bora wa pili (Saa 1:00 usiku)
Desemba 4,
2012
(16:00):
Mshindi
Kundi B vs Mshindi wa Tatu Bora wa kwanza (Saa 10:00 jioni)
Mshindi
wa Pili Kundi A vs Mshindi wa Pili Kundi C (Saa
1:00 usiku)
NUSU FAINALI:
Desemba 6,
2012
Nusu
Fainali ya Kwanza (Saa 10:00 jioni)
Nusu
Fainali ya Pili (Saa
1:00 usiku)
MSHINDI WA TATU:
Desemba 8,
2012
Waliofungwa
Nusu Fanali (Saa 10:00 jioni)
FAINALI:
Desemba 8,
2012
Walioshinda
Nusu Fainali (Saa 1:00 usiku)