John Raphael Bocco 'Adebayor', atatwaa kiatu cha dhahabu CECAFA Tusker Challenge 2012? |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
JOHN Bocco ‘Adebayor’
ameingia kwenye orodha ya wachezaji wanaowania ufungaji bora wa michuano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kufuatia
jana kufunga mabao mawili, Tanzania Bara ikiilaza Sudan 2-0 katika mchezo wa
Kundi B, Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda.
Bocco aliyeifungia
Kilimanjaro Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager mabao yote hayo
kipindi cha kwanza, sasa analingana na washambuliaji wa Burundi, Chris
Nduwarugira na Suleiman Ndikumana, ambao kila mmoja ana mabao mawili pia.
Wengine ambao
hadi sasa kila mmoja amefunga bao moja ni Yussuf Ndikumana wa Burundi, Mohamed
Jabril wa Somalia kwa penalti, Geoffrey
Kizito wa Uganda na Yonatal Kebede Teklemariam.
Bocco ana
nafasi zaidi ya kuongeza mabao katika mechi za kundi hilo, haswa kwenye mchezo
dhidi ya Somalia Desemba 1, kwani hiyo ndio timu dhaifu zaidi kwenye Kundi B.
Lakini Bocco
kama atacheza kwa kiwango cha jana, anaweza akawa mwiba hata mbele ya Burundi Novemba 28.
Kwa sasa
Bocco anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, ndiye mshambuliaji pekee kwenye kikosi
cha Bara, baada ya washambuliaji wengine, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu
wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemomkrasia ya Kongo (DRC) kuzuiliwa na
klabu yao.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
John Bocco Tanzania
2
Yussuf
Ndikumana Burundi 2
Suleiman
Ndikumana Burundi 2
Yussuf
Ndikumana Burundi 1
Mohamed
Jabril Somalia 1(penalti).
Geoffrey
Kizito Uganda 1
Yonatal Teklemariam Ethiopia 1