Abdi Kassim 'Babbi' kushoto ametemwa, Suleiman Kassim 'Selembe' kulia ameitwa |
Na Ally Mohamed, Zanzibar
Siku moja baada ya kuteuliwa na Kamati Tendaji ya Zfa Taifa
kuwa Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes ambayo itashiriki
michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge,
baadaye mwezi huu mjini Kampala, Uganda, Salum Bausi Nassor ametangaza majina
ya wachezaji 26, watakaoanza mazoezi kuanzia Jumanne ijayo.
Akitangaza majina ya wachezaji hao mbele ya waandishi wa
habari katika ukumbi wa Zanzibar Ocean View, Salum Bausi, amesema licha ya muda
mfupi alionao kuandaa kikosi cha ushindani katika mashindano hayo, lakini
amezingati mambo muhimu katika uteuzi huo, huku akisema uteuzi huo
haukuingiliwa na viongozi wa chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar na
kusisitiza suala la nidhamu ndio kigezo cha msingi katika uteuzi huo.
Amewataja waliochaguliwa katika kikosi cha Zanzibar Heroes
kuwa ni:-
Walinda mlango ni; Mwadini Ali (Azam), Suleiman Hamad (Black
Sella), Abdalla Juma (Kipanga).
Walinzi; Nassor Masoud 'Cholo' (Simba), Salmin Haji Nuhu
(Azam), Agrey Moris (Azam), Nadir Haroub Ali 'Canavaro' (Yanga), Aziz Said Ali
(Kmkm), Mohammed Juma Azan (JKU), Ali Mohammed Seif (Mtende Rangers).
Viungo; Hamad Mshamata (Chuoni), Ali Bakar (Mtende Rangers),
Is-haka Mohammed (JKU), Twaha Mohammed(Mtibwa Sugar), Suleiman Kassim 'Selembe'
(Coastal Union), Saad Ali Makame (Zanzibar All Stars), Makame Gozi (Zimamoto),
Issa Othman Ali (Miembeni), Aleyuu Saleh (Black Sella), Abdulhalim Humoud
(Azam), Khamis Mcha Khamis 'Viali' (Azam).
Washambuliaji; Amir Hamad (JKT Oljoro), Jaku Joma Jaku
(Mafunzo), Abdallah Othman (Jamhuri), Nassor Juma (JKU), Faki Mwalim
(Chipukizi).
Wachezaji hao wanatarajiwa kuchujwa wiki ya mwisho kabla ya
mashindano na kubakia wachezaji 20 ambao wanatarajia kuingia kambini kujiandaa
na safari ya kuelekea Kampala, Uganda tayari kwa michuano ya Chalenji.